Kocha wa timu ya Namungo Bakari Malima kutoka Wilaya Ruangwa Mkoani Lindi amejigamba kuondoka na ushindi dhidi ya timu ya Yanga SC ya Jijini Dares Salaam Katika Kombe la Shirikisho la Azam.
Namungo ambayo inaongoza katika msimamo wa Ligi daraja la kwanza inatarajia kucheza na Yanga SC siku ya jumapili wiki hii wakiwa katika muendelezo wa kusaka tiketi ya kusaka tiketi ya kwenda robo fainali.
Malima anasema anaifaham timu ya Yanga Vizuri hivyo anauhakika wa kupata ushindi akiwa katika kiwanja cha Nyumbani. “Mimi Yanga nawafaham nje ndani,sidhani kama watapata mteremko kama wanaotarajia na uhakika kwa kuwa gemu yenyewe tunachezea nyumbani tunauwezo wa kufanya vizuri” amesema kocha Malima.
Licha ya kujiandaa Vizuri timu hiyo inamajeruhi wanne wa kikosi cha kwanza ambapo kocha tayari ameanza kuandaa vijana wengine ili kuweza kuziba pengo la wachezaji hao. “Tatizo lililopo kwenye timu yangu sasa hivi kuna majeruhi kama wanne wa kikosi cha kwanza na niwachezaji tunaowategemea lakini tayari kuna vijana tunawaandaa kuchukua nafasi” alisema Malima
Hata hivyo amewaomba mashabiki wa mikoa ya kusini kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya jumapili na kuishangilia timu ya Namungo kama moja ya timu inayowakilisha mikoa ya Kusini.
Wakati huohuo kikosi cha Yanga kimeingia jijini Dar es Salaam asubuhi ya leo kikitokea jijini Mwanza walipokuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Mbao FC na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, mchezo ambao ulipigwa kweye uwanja wa CCM Kirumba.
Mara baada ya kutua jijini Dar es Salaam kikosi Yanga kimeanza maandalizi kuelekea mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa utakuwa mgumu kwa pande zote mbili.