Sambaza....

Moja ya homa ya homa ya derby ya kariakooo baina ya Yanga na Simba huwa inakuwa ni uamuzi. Nani atatoa hukumu ngumu ambayo ‘mkosemfu ‘huwenda ni mwanafamilia wa ndani kabisaa nawe ,nasema haya kwa sababu kuu moja ni ukweli ulio wazi kuwa familia nyingi za Watanzania zimegawanyika katika ushabiki wa timu hizi mbili Simba na Yanga.

Uteuzi wa Kayoko na wenzake Frank Komba, Mohamed Mkono na fundi mwingine kwenye nafasi hiyo Elly Sasii kuwa kwenye timu ya uamuzi ni chaguo sahihi kwa maono yangu.

Nimemfahamu bwana mdogo Kayoko miaka kadhaa takribani 10 akianza career yake ya uamuzi, nikibahatika kufanya naye kozi ya FIFA kwa pamoja mimi nikifanya Football Coaching yeye akifanya Referee Course za FIFA zilizoendeshwa pamoja mwaka 2014 kama inavyoonekana pichani hapo juu na wenzake wengi wanaochesha kwa sasa ligi kuu Raphael Ikambi.

Wakati huo kikiwa ‘kivulana’ cha chini ya miaka 17 binafsi nilianza kuona uwezo wake desire na determination yake kuja kuwa mwamuzi mkubwa , tukiwa wakweli kupewa game ya kariakoo derby si jambo jepesi

Mwamuzi Ramadhani Kayoko akisimamia mchezo kati ya Yanga na Zanaco ya Zambia.

Kayoko alipita kwenye program halisi za uamuzi pale Twalipo kabla ya kufanya kozi kubwa ya FIFA chini ya instructor Tangawalima kutoka Zimbabwe.

Hakika ni ushindi mkubwa kwa watu waliomuandaa hadi sasa kufikia kukabidhiwa jukumu zito hivyo Mwenyezi Mungu akamtangulie achezeshe game vizuri bila hofu wala mapepe yeyote.

Ramadhani Kayoko (wakwanza kulia) akiwa katikati mwa uwanja katika mchezo kati ya Simba na Yanga.

Wachezaji, mashabiki, viongozi wa pande mbili, viongozi wa shirikisho, mamlaka za uwanja wakamuheshimu dogo huyu bila kujalisha umri wake.

Walatini wanamsemo wao ‘Roma Locuta est finita est’ kesi imeisha ,sawa na kusema maamuzi ya Kayoko ni ya mwisho.

Sambaza....