Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Mtunisia Nasradinne Nabi amesema wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Real Bamako.
Nasraddine Nabi amesema ni muhimu kushinda mchezo wa kesho ili kuendelea kuweka hai matumaini yakufuzu robo fainali.
Nasraddine Nabi “Tumejiandaa vizuri na mechi ya kesho na ili tusonge mbele mchezo dhidi ya Bamako na mchezo unaofuata ni muhimu kushinda maana mchezo wa mwisho utakua mgumu sana.”
Pia kocha Nabi amesema mchezo wa kwanza uliopita kule Mali umewapa morali yakupambana kutokana na kukosa alama tatu dakika za mwishoni.
“Wachezaji wote hawakufurahishwa na matokeo yaliyopita kwenye mchezo wa kwanza dhidi yao ugenini baada ya kuruhusu bao dakika za mwisho na hiyo imewapa morali kipambania matokeo ya kesho,” alisema Nabi.
Yanga wataingia uwanjani kesho saa moja jioni katika Dimba la Benjamin Mkapa kuwakaribisha Real Bamako katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.