Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya Azamsports Federation Cup au kombe la FA baada ya kuitoka Afrikan Sports ya Tanga.

Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa sifuri katika Dimba la Uhuru na kujihakikishia kutinga robo fainali na sasa wanasubiri ratiba tuu.

 

Goli la kwanza la Simba lilifungwa na Jean Baleke dakika ya 36 baada yakupokea pasi safi kutoka kwa Pape Sakho na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele.

Mwanzoni mwa kipindi cha pili Kenedy Juma alifunga bao la pili kwa kosa ya chinichini iliyopigwa na Moses Phiri. Simba waliandika bao la tatu kupitia kwa nyota wake chipukizi Mohamed Mussa baada ya gonga nzuri ya yeye na Moses Phiri.

Mohamed Mussa akifunga bao la tatu la Simba mbele ya mlinzi wa African Sports.

Goli hilo lilionekana kushangiliwa kwanguvu na mashabiki wa Simba kutokana na ufundo mkubwa uliokua unaonyeshwa na Mohamed Mussa aliejiunga tena na Simba dirisha dogo akitokea Zanzibar klabu ya Malindi.

Msumari wa mwisho kwa Simba kwenda kwa Mabaharia hao ulishindiliwa na Jimson Mwinuke baada ya pasi safi kutoka kwa Peter Banda katika dakika ya 90.

Mpaka mpira unamalizika Simba nne Afrikan Sports hawajapata kitu. Katika mchezo huo gumzo kubwa likiwa ni kiwango cha Mohamed Mussa ambae aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya Habib Kyombo.

Simba sasa wanajiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers utakaopigwa wiki ijayo katika uwanja wa Taifa.

Sambaza....