Mwenyekiti wa bodi ya ligi Steve Mguto, amesemakuwa wao kama bodi ya ligi hawajui zawadiatakayopewa mshindi wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu 2018/19 kutokana na kukosekana kwamdhamini.
Mguto amedai kuwa kukosekana kwa wadhaminikunaifanya bodi hiyo kutojua hasa cha kumpa mshindijapo amekiri kuwa, juhudi kubwa zinafanywa na bodihiyo kumtafuta mdhamini atakayetanzua mgogorohuo.
“..zawadi watu watapata na ikifika muda wa kueleza nini tutatoa tutawaeleza tu… wadhamini watapatikanaana zawadi zitapatikana tu kabla ya ligi kuisha, mudahautuachi kwa kuwa na sisi tunakimbizana nao”
“ kwa hili bodi ya ligi hatujayumba, ni kawaida mudamwingine masuala kama haya hutokea”.
Mguto amewatoa hofu wadau wa soka nchini juu yazawadi za mshindi, na kusema kuwa, zawadi lazimaziwepo na juhudi kubwa zinafanywa kuhakikishawadhamini wanapatikana.
Hadi sasa ligi kuu Tanzania bara ipo katika duru la pili, huku timu zote zikijitahidi kupambana kupata matokeoili zingine zisishuke daraja na zingine zikigombaniakumaliza nne bora lakini hadi leo hakuna anayejuatimu hizi zinagombania nini.
Tangu kuanza kwa ligi hiki ndicho kitendawiliambacho bado hakijapatiwa jibu lake. Licha ya timukuteseka hasa kukosa mahitaji mbalimbali kutoka kwamdhamini wa ligi vikiwemo vifaa vya michezo napesa.
Wadau wengi wa soka nchini wanaamini kuwa, kukosekana kwa mdhamini mkuu wa ligi, kunaongezaukata kwa vilabu na hii hurahisha upangaji wamatokeo.