Mwenyekiti wa klabu ya Simba Murtaza Mangungu amesema hawapaswi kupewa pole kwasababu hawajapata adhabu kule Afrika Kusini na kuongeza wanastahili kupongezwa kwasababu wameonyesha uwezo mkubwa katika michuano ya Afrika.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba alizungumzia pia mambo yaliyokua yakionekana yakishirikina katika kipindi cha michezo cha Efm.
“Simba lazima tupewe hongera kwasababu ni timu ambayo inawezo wakusema tunaenda robo fainali na tukaenda kweli.
Watu wa historia wanajua kuelezea vizuri nadhani tangu huko nyuma miaka ya 1960, 1970 tumefika sana hizi hatua kwahiyo nafikiri tunastahili kupongezwa kama Simba.” Murtaza Mangungu Mwenyekiti wa Wanachama wa klabu ya Simba.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba pia amezungumzia pia mambo yaliyoonekana yakihusishwa na imani za kishirikina na kusema haoni kama kuomba dua ni dhambi uwanjani.
“Kuomba dua sijawahi kusikia kama ni dhambi, timu nyingi huwa zinaomba dua hata Berkane walikuja hapa wakazunguka na kuomba dua.
“Kwenye ile video mimi binafsi sikuona moto labda tuu kuna picha zilizotengenezwa zinasambaa.
Kama kweli ule ungekua ni moto unawaka vile basi hata hao wachezaji basi miguu yao ingeungua.” Murtza Mangungu alisema.
Simba iliondolewa katika hatua ya robo fainali katika michuano ya Kombe la Shirikisho na Orlando Pirates kwa penati 4-3 baada ya matokeo ya jumla katika michezo yote miwili kuisha kwa kila timu kupata ushindi wa bao moja bila.