Sambaza....

Kiungo Mshambuliaji Geoffrey Mwashiuya amesema ameshapata ofa kutoka vilabu vitatu mpaka sasa ambavyo vinataka huduma yake katika kipindi hii cha Dirisha dogo la Usajili.

Mwashiuya amesema kati ya vilabu hivyo kimoja ni kutoka nje ya nchini na kwamba kutolipwa stahiki zake na waajiriwa wake wa sasa ambao ni Singida United kunamfanya kufikiria maisha mengine na pengine kujiunga na Klabu nyingine katika dirisha dogo la Usajili.

“Malipo yangu ya usajili sijapewa hadi sasa, Ila maisha ya Singida nimeishi vizuri japo changamoto zipo ambazo ni kawaida kila sehemu unayoenda kufanya kazi, madai yangu ni pesa zangu za usajili sijalipwa Hata senti 50 pamoja na mshahara nadai lakini Uongozi umeniambia nisubiri na ndio maana nasubiri kuona itakuaje,” amesema Mwashiuya.

Akizitaja timu ambazo zimeonesha nia ya kumuhitaji Mwashiuya ameitaja timu yake ya zamani ya Yanga ambayo ndiyo aliacha mwanzoni mwa msimu na kujiunga na Singida United pamoja na Lipuli FC ya Iringa na KCB FC ya Kenya ambayo Jamal Mwambeleko amejiunga nayo akitokea pia Singida United.

“Kuna timu ambazo zinanihitaji katika hili dirisha dogo ambazo ni timu yangu ya zamani Dar Young Africans ambayo inataka kunirudisha, pia Lipuli nimesikia inanihitaji pia timu moja ya Kenya inaitwa KCB nayo pia inahitaji” amesema Mwashiuya ambaye ni zao la timu ya Kimondo FC ya mkoani Songwe.

Sambaza....