Sambaza....

MUZAMIRU Yassin aliingia katika orodha ya viungo watatu bora katika tuzo za Mo Dewji usiku uliopita na licha ya kwamba hakushinda tuzo hiyo iliyokwenda kwa Mghana, James Kotei kiungo huyo wa kati namtazama kama mfano wa kuigwa.

Mwanzoni mwa msimu alipoteza nafasi yake mbele ya Cletus Chama, Jonas Mkude na Kotei ambao kocha Mbelgiji, Patrick Aussems alipendelea kuwatumia zaidi.

Aussems alikuwa akiwatumia zaidi Hassan Dilunga na Said Ndemla kama wasaidizi katika eneo la kati na kuna wakati ilionekana wazi mwisho wa Muzamiru ndani ya klabu ya Simba ulikuwa ukikaribia.

Chama akipiga mpira

Kushindwa hata kuwa sehemu ya wachezaji muhimu wa akiba hakukumvunja nguvu kijana huyo mwenye miaka 23, zaidi aliongeza jitihada katika mazoezi na taratibu mchezaji huyo akaanza kupewa tena nafasi na kila alipokuwa uwanjani alionyesha yupo tayari kubeba majukumu aliyopewa.

Kushindwa kushinda tuzo hiyo hakuwezi kuondoa ukweli kuwa Muzamiru ni kati ya wachezaji ‘wazawa’ ambao walitumia vizuri nafasi finyu waliyopata na kuonyesha thamani yake.

Akitumia nguvu, uwezo wa juu wa kupora mpira, Muzamiru anatakiwa labda kuboresha aina yake ya upigaji pasi, na jinsi ya kushambulia kwa tahadhari hasa dhidi ya wapinzani wakali.

Niyonzima

Kutokushinda tunzo ni jambo lingine, lakini kitendo tu cha kumudu kuwepo katika orodha ya viungo watatu bora wa klabu yake msimu uliopita ni ishara njema zaidi kwake kama ataendelea kujituma na kufuata maelekezo ya walimu wake.

Haruna Niyonzima ambaye alimaliza msimu katika kiwango bora, Chama, Dilunga wote hawa hawakuweza kuingia tatu bora lakini Muzamiru ambaye alianza msimu kama mchezaji asiye na nafasi hata ya kuingia akitokea benchi ameweza kupewa heshima.

Sambaza....