Kama ningeulizwa ya Mtibwa Sugar FC ilipaswa kuwa timu ya mchezo gani basi jibu langu la moja kwa moja ingekuwa Karata.
Hawa ni magwiji wa mchezo ule maaarufu wa karata ‘ last card’ wa kugemua mwisho huku watu wakificha majokers na vimbili’.
Misimu mitatu ya mwishoni mambo yao hayaendi vizuri lakini wamekuwa na ufundi wa kujipapatua mwishoni na majaliwa yao kuamuliwa katika mchezo wa mwisho.
Mfano msimu wa 2019/20 game yao mwisho dhid ya Ruvu shooting ndiyo ilitoa hitimisho lao la kubaki katika ligi kuu.
Msimu wa 2020/21 Mtibwa ililazimika kucheza Play off na Transit Camp ambapo ilishinda mchezo wa kwanza 4-1 uwanja wa Uhuru na baadaye kupoteza 2-1 nyumbani Morogoro.
Msimu huu pia hawakufanya vizuri na kurejea kule walikotoka msimu uliopita wa kucheza Play off dhid ya Tanzania Prisons ambapo katika mchezo wa kwanza wamefanikiwa kushinda 3-1.
Naamini wanakwenda kumalizia robo duara katika mchezo wa pili Manungu Turian na kujihakikishi usalama wa kusalia kwenye ligi kuu ya NBC.
Na hapa kukamilisha dhana ya Mtibwa kuwa Club ya ‘karata ‘huku wakimudu zaidi kucheza mchezo wa ‘last card’ unaohitaji mtu kugemu.
Wamekuwa mafundi sana sana wa kutumia hii nafasi ya pili ya kujiuliza wakicheza kwa nguvu na maarifa tofauti na mechi nyingi zilizopo kwenye msimu ni kama watu wanaochaji jioni.
Yawezekana ‘utambuzi ‘ wa hatari ya kushuka huwa unakuja hapa mwishoni au motisha toka kwa uongozo huwa inakuwa kubwa kwa tafsiri ya ahadi kubwa ya fedha kwenye kuinusuru timu.
Mtibwa ni kama zama zake zimekwisha baada ya ujio wa Azam wakati siku za nyuma hawa ndiyo walikuwa washindani wakweli wa vilabu hivi vya kariakoo.
Na ilifika pahali wanauwezo wakusajili mchezaji aliye kwenye chati katika vilabu hivi kama ambavyo waliwahi kuwasajili akina Dua Said, Mwanamtwa Kihwelu, Monja Liseki, Alphonce Modest nk kwa ushawishi na madau makubwa lakini si kwa sasa.
Mtibwa imeamua kugeuka kama academy ya kutengeneza wachezaji wazuri wa kuzitumikia vilabu vingine kwa mafanikio kama vile msimu huu ambao Yanga wamekuwa mabingwa wametumia wachezaji kadhaa toka timu hiyo.
Dickson Job ,Kibwana Shomary Abutwaalibu Mshery ni sehemu ya ushuhuda wa jambo hili nyuma yake kwenye mafanikio ya Simba Ramadhani Kichuya, Mohammed Ibrahim ‘Mo’ na Mzamiru Yasini ambaye hadi leo yupo pale anaunguruma dimbani.
Nini mnakwama Mtibwa Sugar, amkeni katika usingizi mzito mje mudishe hadhi ya klabu hiyo iliyojengwa vizuri mwishoni mwa miaka ya 1990.
Bila kufanya hivyo kuna siku Mwenyezi Mungu hata sikiliza maombi yenu na nafasi hiyo atawapa wengine Amken sasa mabingwa wa ‘last card’.