Sambaza....

Kwa mujibu wa mtandao wa Bingwa inaonesha ndoto za winga wa zamani wa Yanga, Simon Msuva za kucheza soka la kulipwa Ulaya, zinakwenda kutimia baada ya dili lake na klabu ya Benfica inayoshiriki Ligi Kuu Ureno, kukamilika.

Msuva kwa sasa anakipiga katika timu ya Difaa El-Jadida ya Ligi Kuu ya Morocco, iliyomsajili mwaka 2017 kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Yanga.

Akizungumza na BINGWA jana, Meneja wa mchezaji huyo, Dkt. Jonas Tiboroha, alisema Msuva anatarajia kujiunga na timu hiyo Januari mwakani na kwamba makubaliano yao itamtoa kwa mkopo wa miezi sita kwenda Panathiakos ya Ugiriki.

“Janauri mwakani huenda Msuva akawa katika timu ya Panathiakos, atacheza kwa mkopo wa miezi sita baada ya kusajiliwa na Benfica,” alisema Dkt Tiboroha.

Tangu amejiunga na Difaa el Jadida, Msuva amekuwa na kiwango kizuri muda hasa katika upachikaji mabao, akiwa ni msaada mkubwa kwa timu hiyo, hali iliyomfanya afukuziwe na klabu nyingi, ikiwamo Malaga ya Hispania.

Hata katika timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Msuva amekuwa kati ya wachezaji tegemeo kutokana na kujitoa kwake uwanjani.

Sambaza....