Msimu ujao Yanga Msimu wa soka Tanzania bara umekamilika baada ya kushuhudia mechi ya fainali ya Azam Federation Cup kati ya Namungo FC na Simba katika uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga Rukwa.
Katika fainali hii tumeshuhudia Simba akishinda goli 2-1 na kuchukua ubingwa wa Azam Federation Cup na kufanya wabebe vikombe vitatu msimu huu ambavyo ni ngao ya jamii , ligi kuu Tanzania bara pamoja na kombe la Azam Federation Cup.
Baada ya mchezo huu Afisa Habari wa Simba , Haji Manara alidai kuwa Simba haistahili kucheza kwenye nchi hii na inacheza tu kwa sababu Tanzania ni nchi yao.
“Nina ubingwa wa FA , ligi kuu , ngao ya jamii . Yanga nimempiga nne , anayefuatia nimempiga huyo Namungo FC nimempiga naye hii ni Simba inacheza kwenye viwanja vibovu na vizuri huku ikishinda.
“Sisi hapa Tanzania hatutakiwi kucheza , tunatakiwa kucheza kwa wenzetu wanaojua . Tunacheza hapa Tanzania kwa sababu ni nchi yetu Ila hatutakiwi kucheza hapa”- alisema Haji Manara.
Kuhusu msimu ujao Haji Manara amedai kuwa Yanga wanatakiwa kujiandaa kwa sababu msimu ujao atawafunga goli kumi.
“Acha wasajili , Msimu uliopita walisajili wachezaji 24, nikawapiga 4 basi msimu ujao nawapiga 10. Acheni wasajili , usajili siyo kukurupuka ndiyo maana sisi tumekaa kimya”- alisema Haji Manara