Kamati ya maadili ya shirikisho la mpira Tanzania TFF limemfungia kutojihusisha na mchezo wa soka maisha msimamizi wa kituo cha Mtwara Dustan Mkundi kwa kughushi na udanganyifu wa mapato ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya wenyeji Ndanda FC dhidi ya Simba sc ikiwa ni kwenda kinyume na kanuni ya 32(2) na ile ya 32(4)
Kamati hiyo iliyoketi leo hii kwenye ofisi za shirikisho hilo la soka nchini, zilizopo Ilala jijini Dar es salaam
Imemfungia miaka mitano Katibu mkuu wa Chama cha mpira wa Miguu mkoa wa Mtwara Kizito Mbano kwa mujibu wa kanuni za maadili za TFF kifungu cha 73(7) huku ikimpa onyo Katibu msaidizi wa Ndanda Seleman Kachele
Pia kamati hiyo haitoendelea kusikiliza shauri dhidi ya muhasibu wa msaidizi wa Simba Suleiman Kahumbu baada ya Sekretarieti ya shirikisho hilo kutoendelea na shitaka dhidi yake
Katika mchezo huo ambao Simba waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 huku ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu kwa kocha Masoud Djouma kukiongoza kikosi hicho baada ya aliyekuwa bosi wake Joseph Omog kutimuliwa