Sambaza....

Baada ya mlipuko wa ugonjwa wa corona kuitikisa dunia tangu ulipotolewa taarifa kuisumbua nchi ya China na kuenea katika nchi mbalimbali duniani na pia umepelekea mchezo wa soka pia kuathirika.

Baada ya ugonjwa huo kuingia nchini Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa alitoa taarifa ya kusimamisha michezo yote kuanzia Ligi Kuu mpaka Ligi  daraja la Pili.

Baada ya katazo hilo la kuendelea na Ligi Kuu Bara miongoni mwa wachezaji walioathirika na ligi kusimama ni mshambuliaji wa pembeni wa Alliance fc  David Richard Uromi anaeitumikia klabu hiyo ya kanda ya ziwa.

David Richard ni miongoni mwa wachezaji waliofunga “Hatrick” msimu huu.

Tovuti ya Kandanda iliweza kupata maoni ya David Uromi  kuhusu ugonjwa wa corona ambae ni moja kati ya wachezaji 6 walioweza kufunga magoli matatu katika mchezo mmoja “Hatrick” katika VPL msimu huu.

David Uromi “Ni ugonjwa hatari kwa sasa duniani ni janga la Kidunia kikubwa sisi kama watanzania tuchukue tahadhari tulizopewa na wataalam wa afya “tusipanic” tuchukue tu tahadhari maana kinga ni bora kuliko tiba.”

David pia alizungumzia matokeo ya kusimama kwa Ligi Kuu Bara na afya za wachezaji na mashabiki wa soka pia.

David Richard Uromi

David Uromi “Sioni kama kusimama kwa Ligi  kuna athari sana maana afya ni bora kuliko kucheza. Lazima tukubaliane na mazingira kwa sasa hali hairuhusu tusubiri tamko la Serikali hadi litakaporuhusu. Kwa timu gharama za uendeshaji zinakuwa kubwa kwasababu wanakuwa tayari na bajeti yao ya msimu mzima.”

Kuhusu kusimama kwa Ligi na madhara ambayo watayapata kama wachezaji David alisema hawatokaa nyumbani bure ni lazima wafanye mazoezi binafsi haswa wao Allianve kutokana na nafasi waliyopo katika Ligi.

“Sisi kama wachezaji tunathamini kazi yetu na ukizingatia team yetu haipo katika hali nzuri tunahitaji kuibakiza katika ligi kila mmoja atafanya mazoezi atakapokuwa ili tutakaporudi tufanye vzuri katika ligi na kuweza kubaki Ligi Kuu Bara.”

Sambaza....