Msemaji wa Azam Fc Zakaria Thabir anaendelea kuandika jinsi ambavyo kauli ya kupania kwa timu yake ya Azam Fc ilivyokua na pande mbili kwa timu hiyo tajiri kutoka Chamanzi jijini Dar es salaam.
Zaka za Kazi anabainisha katika toleo lake la pili baada ya lile lakwanza kulisema katika matokeo chanya, sasa anauelezea upande wa pili akisema “Kwenye kila baya kuna jema ndani yake, ndivyo inavyotufundisha Quran Tukufu. Na hata kwenye kauli mbaya ya Mayele kuhusu wachezaji wa Azam FC kukamia dhidi ya Simba na Yanga na kujilegeza dhidi ya akina Namungo, ina ujumbe mwema ndani yake, kama nilivyoutafsiri kwenye andiko lililopita,”
“Kwenye andiko hili, naangalia upande wa pili wa kauli hiyo, yaani upande wa ubaya.
Mayele, wachezaji wa Azam FC wanajitoa kwa uwezo wao dhidi ya timu zote wanazokutana nazo, tofauti ni kwamba kuna vitu wanakutana navyo ambavyo wewe hukutani navyo.”
Zaka anasema kuwepo Azam kama mchezaji na kushinda mechi si jambo jepesi kama ambavyo Mayele amesema na kumpa ushauri atawaulize wachezaji waliotoka Azam ambao sasa wapo Yanga.
“Kuna wachezaji kadhaa waliokuwa Azam FC ambao sasa uko nao hapo UTOPOLONI, hebu waulize hali ikoje kuichezea Azam FC. Msimu uliopita kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City, wewe ulinyimwa nafasi moja ya kufunga kwa kuhukumiwa umeotea ilhali haikuwa hivyo. Ile nafasi moja iliwaibua wazee wa klabu yenu, viongozi wa dini na hadi wanasiasa wenye dhamana ya kitaifa,” alisema kuongeza
“Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba, akiongea kwa niaba ya serikali, alisema wataleta VAR kwa sababu Yanga inaonewa sana. Sasa tukio kama lile ndiyo maisha ya kila siku ya wachezaji wa Azam FC. Wewe una bahati unachezea klabu ambayo ikiguswa kidogo, hadi viongozi wa dini wanatikisika, kwa hiyo kuna vitu vingi sana hukutani navyo…ndiyo maana unaleta dharau dogo.
Narudia tena, ongea na Sure Boy akuhadithie maisha halisi ya kuichezea Azam FC. Ongea na Mudathir Yahya akueleze nini ugumu wa kuichezea Azam FC. Hivyo vigoli vyako 16, sasa hivi ungekuwa navyo 6 au 7….usifanye mchezo.”