Sambaza....

Baada ya kumtimua kocha wake Jose Mourinho, klabu ya Manchester United imemtangaza rasmi mrithi wa mikoba ya mreno huyo Old Traford.

Jana jumanne Man U ilimtambulisha  Mnorway na mwanandinga wa zamani wa mashetani hao, Ole Gunnar Solskjaer kuwa mrithi wa Mourinho kama kocha wa muda hadi pale timu itakapotangaza kocha wa kudumu katika majira ya kiangazi.

Utambulisho huo, ambao ulifanyika jana jioni kimakosa katika tovuti ya timu ulifutwa baada ya masaa kadhaa. Man U waliweka video ikimuonesha Solskjaer akifunga goli katika fainali za klabu bingwa barani ulaya mwaka 1999 dhidi ya Baryen Munich, huku video hiyo ikifuatiwa na maneno yanayosomeka hivi,

“Solskjaer ndiye kocha wetu wa muda, ni misimu 20 sasa bado tunalikumbuka hili goli katika uwanja wa Nou Camp”

Ole akishangilia wakati akiichezea United.

Baada ya utambulisho huo wa kimakosa katika tovuti ya klabu, waziri mkuu wa Norway, Erna Solberg kupitia kurasa zake za kijamii alimpongeza Solskjaer na kumkaribisha katika majukumu yake mapya kama kocha wa muda wa Man U, na kudai kuwa,kuteuliwa kwake ni fahari kubwa kwa taifa na maendeleo ya soka nchini Norway nakisha kumtakia mafanikio mema, lakini baada ya muda naye alifuta bandiko lakehilo katika ukurasa wake.

Solskjaer mwenye miaka 45, aliichezea Man U kwa misimu 11 na kuifungia magoli 126 kama atateuliwa kuwa kocha wa muda, mechi yake ya kwanza itakuwa ni dhidi ya Cardiff city jumamosi hii.

Sambaza....