Taarifa za ndani ya Yanga zinaonesha tayari mazungumzo kati ya David Molinga na Yanga kuhusu kuvunja mkataba wake yamefikia sehemu ambayo ni nzuri.
Pande zote zimefikia katika hatua ambayo ni nzuri ,makamu mwenyekiti wa Yanga, ndugu Fredrick Mwakalebela amedai kuwa mpaka sasa wako kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba na David Molinga.
“Tuko kwenye mazungumzo mazuri ya kuvunja mkataba na David Molinga , mpaka sasa hivi mazungumzo yetu yamefikia sehemu ambayo ni nzuri.”alisema makamu mwenyekiti huyo wa Yanga.
Kuhusu mchezaji ambaye anatakiwa kuja kuziba nafasi ya David Molinga mpaka sasa amedai kuwa wamefikia kwenye hatua ambayo ni nzuri.
“Mpaka sasa hivi Tumefikia hatua nzuri ya kumtafuta mchezaji ambaye ni Mrithi wa David Molinga , tuna nafasi mbili za kujalizia kwa hiyo tutazitumia ipasavyo” alimalizia Mwakalebela.
Mpaka sasa hivi Yanga imeachana na baadhi ya wachezaji wa nje waliosajiliwa na Mwinyi Zahera kama Juma Balinya ,Issa Birigimina , Sadney .