Manchester United wamesukumwa nje ya michuano ya Uefa Champions league, hii ndio lugha nzuri unayoweza kuitumia, katika mchezo ambao Sevilla wameondoa lile jinamizi baya la kutofanya vizuri kunako ardhi ya malikia
Ndio Sevilla wamefanikiwa kuondoa jinamizi, kwa maana hapo kabla walicheza michezo minne nchini Uingereza wakiambulia sare tatu na kufungwa mmoja, lakini hapo jana walifanikiwa kupata ushindi wao wa kwanza kwa kuichapa Manchester United mabao 2-1
Ukiwa ni mchezo wa pili kwa Manchester United kupoteza kwenye hatua hii, dhidi ya timu kutoka nchini Hispania ukitangulia dhidi ya Real Madrid msimu wa 2012/13, ukiwa ni mchezo wa 6 kwa kocha Jose Mourinho kupoteza akiwa nyumbani dhidi ya timu kutoka Hispania
Wissam ben Yedder amefunga mabao 2 hiyo jana, sasa anafikisha mabao 8 kwenye Uefa Champions league yanamfanya kuwa mfungaji namba mbili kunako michuano hiyo nyuma Cristiano Ronaldo
Hizo ni rekodi, lakini tukirudi kwenye mchezo wenyewe kwa maana ya tathimini, Jose Mourinho ni kama alijikaanga mwenyewe kwa mafuta yake
Mourinho aliingiza United kwa kutumia mfumo wa 4-2-3-1 Unconventional Formation, moja kati ya mifumo bora kwa sasa na sifa kubwa ya mfumo huu ni kuaribu mfumo wa uchezaji wa timu pinzani, pia ni flexible formation kurudi kwenye 4-3-3 au mfumo mwingine
Sasa kwa nini nasema Mourinho alijikaanga, uteuzi wa mfumo na upangaji wa kikosi hii ni sehemu ya kwanza aliyoanzia kufeli, kwenye mfumo wa 4-2-3-1 unapunguza matumizi makubwa ya kiungo wa kati lakini ukihitaji kiungo mwingine juu atakayecheza kama deep playmaker Mourinho akuanza na kiungo wa aina hii
Nemanja Matic na Maloane Fellain walicheza pamoja kama viungo wa ulinzi (Double pivot)hapa ilikuwa sawa, lakini huku juu yao walicheza Jesse Lingard, Alexis Sanchez na Marcus Rashford hapa ndio kulikuwa na tatizo kwa maana ya kukosa namba 10, halisi ambaye angeweza kuratibu mashambulizi ya timu, lakini pia kusimama kama kiungo wa tatu ambaye angeweza kuisaidia United kushinda vita kwenye eneo la kiungo
Ilikuwa lazima kwa Rashford au Lengard mmoja kuanzia benchi ili nafasi yake angeanza Paul Pogba, huyu ndiye mtu sahihi ambaye angeweza kuisukuma timu mbele kushambulia na kuifanya timu kuwa brast kutokea katikati kiwanja, kitendo cha kumuanzisha benchi Pogba hii ilikuwa ni sehemu nyingine iliyochangia kufeli
Wakati mwingine ni vizuri kuamini kile unachokiamini, lakini kuamini kuwa Sanchez anaweza kucheza nyuma ya mshambuliaji wa mwisho haya ni makosa mengine ya Mourinho, Sanchez sio aina ya kiungo mwenye uwezo wa kutembea na mipira kwa umbali mlefu kutokea kati ya kiwanja na kuichezesha forward line, Sanchez anakuwa bora akitokea pembeni kwa maana ya kusaidia sana kukimbiza mipira kwenye eneo la mwisho
Kwa nini Sevilla walifanikiwa
Katika kitu ambacho Sevilla kwao kimesimama kama siraha kubwa ni kucheza katika mchezo wao uleule, mara zote katika michezo yao wamekuwa na Same approaching game mentality hii imewasaidia sana kwenye mchezo wa jana
Idara yao ya kiungo hii imekuwa ikifanya kazi kubwa sana, Ever Banega, Stephen Nzonzi na Franco Vasquez wamekuwa na muunganiko bora katikati ya kiwanja na ukirejea katika mchezo wa jana hakukuwa na vita kubwa katikati ya kiwanja muda mwingi walicheza kwa uhuru na kufikilia namna ya kumaliza mchezo