Klabu ya Simba imekutana na adhabu kutoka kwa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) baada ya kukutwa na tuhuma za kujihusisha na mambo ya kishirikina.
Katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Orlando Pirates na Simba, wachezaji wa Simba walionekana wakizunguka katikati mwa uwanja huku moshi ukionekana ukitoka katikati yao.
Katikati ya miguu ya wachezaji kulionekana moto ukiwaka huku wao wakionekana kuuzunguka wakirukaruka kupasha miili joto.
CAF imeitoza klabu ya Simba dola 10,000 za Kimarekani (Zaidi ya milioni 23) za Kitanzania baada ya kuthibitika tukio haliendani na maswala ya soka likiwa linahushiwa na mambo ya kishirikina.
Simba iatapaswa kulipa pesa hizi ndani ya siku 60 tangu kutoka kwa hukumu hiyo, lakini pia wana siku tatu za kukataa rufaa kwa hukumu hiyo.
Katika mchezo huo uliishia kwa Simba kuondoshwa katika michuano hiyo kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kumalizika kwa Orlando kushinda bao moja bila na hivyo kupelekea kua sare kwa matokeo ya jumla.