Huku kocha Nasreddine Nabi akihusishwa na Kaizer Chiefs, nyota wa zamani wa PSL Bernard Morrison amefanya ulinganisho wa kuvutia kati ya Amakhosi na Wananchi.
Kaizer Chiefs imesalia kuwa miongoni mwa timu zinazofuatiliwa zaidi katika DStv Premiership. Hata hivyo, mshambuliaji wa Ghana Bernard Morrison ana maoni kwamba Yanga ina ufuasi mzuri kuliko ule wa Kaizer.
Morrison alikaa Afrika Kusini kwa miaka miwili huko Orlando Pirates kabla ya kuachiliwa mnamo Julai 2018.
“Takwimu ambazo klabu [Yanga SC] inazo ni zaidi ya Kaizer Chiefs. Kwenda Kaizer Chiefs kunakuja na presha yake,” Morrison aliambia FARPPost.
“Lakini kama mchezaji, lazima ujitoe. Kuchezea vilabu vikubwa maana yake ni lazima uwe tayari kwa kila jambo. “Kama unahama kutoka Young Africans na kwenda Afrika Kusini kuchezea Kaizer Chiefs, lazima uwe tayari. Kwangu mimi nadhani presha zaidi iko hapa Yanga karibu sawa kidogo na ile ya Kaizer Chiefs.”
“Hata Kaizer Chiefs wanapokwenda kucheza ugenini, hawapati mashabiki wengi uwanjani kama huku. Lakini hapa (Yanga) unapata nambari kubwa ya mashabiki kila wakati unapoenda kwenye mechi. Lazima uwe tayari.”
Nyota wa zamani wa PSL, Bernard Morrison alizungumza na FARPPost kuhusu ushindi wa Yanga dhidi ya Azam FC kwenye Kombe la Shirikisho na kuhitimisha jumla ya mataji matatu msimu huu. Kwa upande wa mafanikio Young Africans SC ina mataji mataji 29 ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Pia Yanga imeshinda idadi kubwa ya vikombe vya ndani pamoja na mataji matano ya kombe la CECAFA. Chini ya kocha Nasreddine Nabi, walishinda mataji sita katika misimu miwili, kipindi ambacho Kaizer haikua inafanya vyema katika Ligi ya PSL.
Yanga pia walikosa kombe la CAF Confederations Cup baada ya kufungwa na USM Alger katika fainali iliyochezwa kwa mikondo miwili kwa jumla ya matokeo ya 2-2 na kukosa kombe kwa bao la ugenini.