Wiki iliyopita baada ya Bernard Morrison kutopokea simu ya kocha mkuu wa Yanga , Luc Eymael na kushindwa kwenda Shinyanga kwa ajili ya mechi dhidi ya Mwadui FC kuliibuka na tetesi nyingi za Bernard Morrison kwenda Simba.
Tetesi ambazo zilikuwa na tairuki kubwa sana kwa mashabiki wa Yanga kwa sababu Bernard Morrison amekuwa kipenzi kikubwa kwa mashabiki wa Yanga kipindi hiki , hivo tetesi hizi zilileta hali ya sintofahamu kwenye kikosi cha Yanga .
Moja ya kiongozi wa GSM , Injia Hersi Said amedai kuwa Bernard Morrison ana mkataba na klabu ya Yanga , mkataba ambao unadumu kwa miaka miwili kwa sasa hivo ni mali halali ya Yanga kwa sasa.
“Ana mkataba wa miaka miwili ambao unaanza Kutumika kuanzia tarehe 14 mwezi wa saba mwaka huu wa 2020. Hivo timu yoyote inayomtaka Bernard Morrison unatakiwa izungumze na Yanga kwanza” – alisema Injinia Hersi Said.
Hersi Said amesisitiza kuwa mpaka sasa hivi hakuna barua yoyote ya kiofisi kutoka Simba iliyokuja Yanga kwa ajili ya Simba kumtaka Bernard Morrison ili awatumikie Simba .
” Kwa maana hiyo Bernard Morrison ni mchezaji halali wa Yanga na Simba kama wanataka kumsajili wanatakiwa kuwasiliana na Yanga, lakini mpaka sasa hivi hakuna barua yoyote kutoka Simba ambayo inamtaka Bernard Morrison”
Kwa mujibu wa Injinia Harsi said , Yanga waliingia na Bernard Morrison mkataba wa miezi aura awali kwa makubaliano ya kuongeza mkataba , baadaye wakaongeza tena mkataba wa miaka miwili .
“Awali tulikubaliana tuingie mkataba wa miezi sita , tulikubaliana naye kuwa kama ataonesha kiwango kizuri tutamuongezea mkataba , mkataba ule wa awali wa miezi sita unaisha tarehe 14/07/2020. Kwa hiyo Ana mwezi mmoja wa kuitumikia Yanga”.
“Baada ya kuonesha kiwango kizuri ndani ya miezi mitatu tu tuliamua kumuongezea mkataba wa miaka miwili ambao utaanza rasmi tarehe 14/07/2020.”- alimalizia injinia Hersi Said