Kwenye mazungumzo ya Leo kati ya Global Online TV na aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga , Mwinyi Zahera amedai kuwa hashangazwi na kiwango cha David Molinga kuwa na magoli 7.
Kwake yeye siyo kitu cha ajabu kumuona David Molinga akiwa ndiye mchezaji anayeongoza kwa kufunga magoli mengi katika timu ya Yanga kwa sababu kilikuwa kitu ambacho alikuwa anakitegemea.
“Nilisema David Molinga atafunga magoli 15 kwenye msimu kwa sababu najua kiwango chache vizuri. Mchezaji siku zote ni takwimu , Mimi niliona takwimu za David Molinga kabla sijamsajili Yanga”.
Kocha huyo aliongeza kuwa kabla ya kumsajili Yanga alikuwa ni mfungaji bora wa pili kwenye ligi ya Congo.
“Alikuwa anaongoza kufunga magoli kwenye ligi ya Congo baada ya Jackson Muleka. Mimi nilikuwa najua kuna siku atakuja kuanza kufunga tu “- alisema kocha huyo.
Kocha huyo pia aliongeza kuwa kitu pekee ambacho kilikuwa kinahitajika kwa David Molinga ni yeye kupata mechi nyingi mwanzoni mwa msimu kwa sababu hakuwa kwenye pre-season.
“Hakuwa na sisi kwenye Pre-season, alihitaji kupata mechi nne mfululizo tu ili aweze kurudi kwenye kiwango chake kama kile alichokuwa nacho Congo”-alimalizia kocha huyo mwenye maneno mengi