Katika kipinedi cha Sports Arena cha Wasafi FM, mwenyekiti wa bodi ya wakuregenzi ya Simba Mohammed Dewji alidai kuwa moja ya sababu ambazo zilisababisha kufukuzwa kwa aliyekuwa mtendaji mkuu wa Simba, Senzo Mbatha ni ongezeko la matumizi ndani ya klabu.
Mohammed Dewji alidai kuwa mkurugenzi huyo mtendaji hakuuingiza fadia yoyote zaidi ya kuongeza matumizi ambayo alitakiwa kuyajibu kwenye bodi ya wakurugenzi lakini akaamua kuondoka kabla hajajibu suala hili mbele ya bodi ya wakurugenzi wa Simba.
Senzo Mbatha amerejea nchini rasmi kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya majukumu mapya ndani ya klabu ya Yanga kama mtendaji mkuu kivuli wa klabu hiyo.
Akiwa katika uwanja wa ndege as kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar Es Salaam amedai kuwa maneno aliyasema Mohammed Dewji ni ya uongo na hamtendei haki.
“Kama kasema hivo basi hanitendei haki kwa sababu niliwasilisha taarifa ya mapato na matumizi kwenye bodi na yeye taarifa hiyo anayo kwenye meza yake.
“Tuliandaa bajeti ya msimu mzima , na mimi nikawa nafanya kulingana na bajeti iliyopo na kwa bahati nzuri msimu umeisha nikiwa nimeokoa baadhi ya pesa ndani ya bajeti. Kama amesema hivo basi hanitendei haki”- alisema Senzo Mbatha alipokuwa anazungumza na mtandao huu kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa