Baada ya ratiba ya Ligi Kuu Bara kutoka hapo jana mchezo wa kwanza kabisa kupigwa utakua ni wa kiporo kati ya Mwadui fc na Yanga katika dimba la Kambarage huko Shinyanga.
Mwadui fc wanakwenda kuikaribisha Yanga siku ya Jumamosi tarehe 13 na tayari vikosi vyote vimeingia kambini tayari kabisa kwa maandalizi. Kocha anaekaimu kwasasa katika klabu ya Yanga Charles Mkwassa amesema kikosi chake kipo tayari na watakwenda kupata ushindi Shinyanga.
Mkwassa “Tunajua mechi itakua ngumu lakini sisi tumejiandaa Yanga ni timu kubwa na ina mashabiki wengi tuna imani tutapata matoekeo mazuri na ndio lengo letu.
Changamoto zipo ndogondogo za injuries kidogo zinasumbua lakini vijana wako katika hali nzuri na changamoto zinapungua, vijana wanafanya mazoezi ya kweli nina imani tutafanya vizuri katika mchezo wetu.
Hakuna minong’ono ya aina yoyote wafanyakazi tunafanya kazi vizuri. Wachezaji wako vizuri na wanaendelea vizuri wapo wenye maumivu madogo tu lakini sio kwa kiasi kikubwa sana.”
Mpaka sasa Charses Boniface Mkwassa anasimana kama kocha mkuu baada ya kocha Luc Aymael kushindwa kufika nchini mpaka sasa kutokana na nchini kwao Ubelgiji kufunga mipaka hivyo kushindwa kusafiri. Lakini uongozi wa Yanga umesema utahakikisha kabla ya Ligi kuanza kocha mkuu Luc atakuepo nchini.
Yanga inakwenda kucheza na Mwadui ambayo ndio klabu yakwanza kuifunga Simba msimu huu katika dimba la Kambarage kwa ushindi wa bao moja kwa bila.