Kocha msaidizi wa timu ya Wananchi Charles Boniface Mkwasa ameweka wazi malengo ya timu yao kwa msimu huu huku pia akiitangazia vita klabu ya soka ya Namungo fc kutoka Lindi.
Yanga baada ya kutoka suluhu na Azam fc katika mchezo wao wa mwisho wa VPL sasa wanakwenda kukutana na Namungo Fc ambao pia ni washindani wenzao katika kuwania nafasi ya pili katika Ligi, ambapo kocha msaidizi Mkwassa amesema wapo tayari kubeba alama tatu ili waweze kusonga mbele.
Charles Mkwasa ” Moja ya shabaha yetu katika mchezo wa kesho ni kuhakikisha tunapata alama tatu ili tusonge mbele zaidi na tukae nafasi ya pili.”
Kwenye msimamo mpaka sasa Yanga wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 56 huku Namungo fc wakifwatia katika nafasi ya nne wakiwa na alama 54 baada ya kuwafunga Kagera Sugar mabao mawili kwa sifuri katika mchezo wao wa mwisho katika uwanja wa Majaliwa Lindi.
Katika mchezo huo utakaopigwa siku ya June 24 Jumatano usiku katika uwanja wa Taifa Yanga sc wametangaza viingilio ambavyo vitakua ni Sh 5,000/= mzungungo, 10,000/= VIP B&C na 15,000/= VIP A.