Simba na Yanga wapo katika visiwa vya Zanzibar wakishiriki katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo timu zote jana zimefanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Wakati michuano hiyo ya kombe la mapinduzi ikiendelea, jana shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF) lilitoa tunzo za kocha bora wa mwezi wa 12 na mchezaji bora wa mwezi wa kumi na mbili.
Katika tunzo hizo , mchezaji wa Simba , Francis Kahata amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya Tanzania kwa mwezi wa kumi na mbili (12) akiwashinda Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union na Hassan Dilunga wa Simba.
Huku kwa upande wa kocha , kocha wa muda wa Yanga Charles Boniface Mkwasa “Master” amefanikiwa kuchukua tunzo ya kocha bora wa mwezi wa kumi na mbili.
Charles Boniface Mkwasa amewashinda Juma Mwanguda wa Coastal Union na Sven wa Simba. Katika mwezi wa kumi na mbili Boniface Charles Mkwasa amefanikiwa kushinda mechi mbili na kutoka sare mechi moja.
Alitoka sare na Mbaya City (0-0), akaifunga Prisons (1-0) na akaifunga biashara United (1-0). Wakati Sven kwenye mwezi wa kumi na mbili amefanikiwa kushinda mechi zote tatu na kufunga magoli 8.
Aliwafunga lipuli (4-0) , akawashinda KMC magoli (2-0) na kuwafunga Ndanda FC magoli (2-0) unadhani Sven anastahili kuwa kocha bora kutokana na matokeo haya ? Yapi maoni yako.