Nimesoma mahala tofauti tofauti wameripoti kuwa Jonas Mkude amemalizana na Yanga SC. Amepewa mkataba wa mwaka mmoja. Bado niko gizani juu ya taarifa hii. Lakini kama kweli Mkude amesaini Yanga SC ataenda kuwanufanisha katika vitu vingi.
Uzoefu, ubora katikati ya kiwanja, uongozi. Hivi ni vitu anavyoweza kuwapa Mkude Yanga SC akiwa ndani ya timu yao. Tanzania haina wachezaji mahiri kwa sasa. Wachache wazawa wako Simba SC, Yanga SC na Azam FC. Ligi yetu haina tena mchezaji kutoka timu za daraja la kati akaja kupata nafasi ndani ya timu kubwa.
Wachezaji wa mwisho kutoka timu za madaraja ya kati kupata nafasi timu kubwa ni hawa wakina Kibwana Shomari, Dickson Job, Dennis Kibu.
Wengine wote waliosajiliwa wamejikuta ni Squad player. Ni kama Dickson Ambundo na Nassor Kapama. Mwisho wa siku huwa wanarudi walikotoka.
Mudathir Yahaya, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’ wameweza kupenya kiurahisi katika kikosi cha kwanza cha Yanga SC kutokana na quality waliyotoka nayo Azam FC. Ni kama nyakati zile Simba SC ilipowasajili kwa pamoja kina Manula kutoka Azam FC.
Binafsi naamini kuna kitu Mkude anakwenda kukifanya na Yanga SC. Anayo quality ya kupambania nafasi. Sio mchezaji mchanga.
Wachezaji wa timu za madaraja ya kati wana mengi ya kujifunza wakisajiliwa Simba SC, Yanga SC na Azam FC kabla hawajapata nafasi ya kucheza vikosi vya kwanza.
Wengi hujikuta katika mazingira magumu na kuamua kurudi walikotoka. Ni wachache waliotoboa. Yanga SC wamerahisisha maisha kumfuata Mkude kama inavyosemekana.