Sambaza....

Jonas Gerald Mkude mtoto wa Kinondoni rafiki Mkubwa wa ndugu yangu Abdul Mkeyenge. Ameufanya mpira uonekane kitu kirahisi ambacho kila mtu atamani kuucheza.

Ndio Jonas Gerald Mkude kiungo mkabaji wa SimbaSc ambae kwa sasa yupo kwenye ubora wake. Kiungo mkabaji wa kisasa tunaweza kumuita, anakaba, anatuliza timu, anaanzisha mashambulizi, mtaalamu wa  kupiga pasi ndefu na fupi yaani  ”A complete defensive midfilder”.

Toka anapandishwa kutoka kikosi B cha Simba msimu wa 2011 Mpaka leo akiendelea kukitumikia kikosi cha Wekundu wa Msimbazi. Ameweza kumaintain nakua katika kiwango bora na cha hali ya juu  mpaka sasa. Na ni moja kati ya viungo bora wazawa mpaka sasa wanaotamba kwenye VPL akiwa na Simbasc.

Kila siku kila msimu Jonas Mkude anazidi kukomaa na kujiimarisha katika eneo la kiungo na kumfanya kua tofauti na viungo wakabaji wengine kama kina Himid Mao wa Azam fc Said Makapu wa Yanga.

Image result for Jonas Mkude images

Modern Defensive Midfielder

Jonas Mkude anacheza kiungo wa ulinzi kama ambavyo dunia ya leo inavyotaka. Kiungo namba sita wa dunia ya leo ndio mwanzilishi wa mashambulizi na ndio muunganishi wa timu pale inapopokonya mpira kwa adui na kuanza mipango ya kushambulia.

Jonas amekua akicheza soft pale timu ikifanikiwa kuuchukua mpira kwa adui na kuanza kushambulia kwa utulivu kabisa, huku akitumia nguvu  mara chache pale inapohitajika na wakati mwingine kupata kadi ya njano kwaajili ya timu pale inapobidi.

Kiungo Mtulivu  Asie na Papara

Moja ya vitu vinavyompa sifa kubwa na kumtofautisha na viungo wengine wa ulinzi ni utulivu wa hali ya juu pale timu yake inaposhambuliwa pia inapokua na mpira. Amekua namba sita asiekua na papara pindi akipewa mpira na mabeki wake hata anapokua na mazingira magumu ya kuzungukwa na adui.

Kwa aina ya uchezaji na utamaduni wa pasi kwa Simbasc pia umemfanya kuwa hivyo mtulivu na kua mchezaji muhimu kwa kuunganisha timu na kuanzisha mashambulizi  kwa pamoja.

Kiongozi Ndani ya Uwanja

Hili lilithibitika pale uongozi wa klabu ya Simba ulipoamua kumpa unahodha ndani ya klabu hiyo na kuitendea haki nafasi hiyo pale alipobeba kombe la shirikisho msimu uliopita. Amekua akihamasisha na kupandisha morali ya timu mara kwa mara wapo uwanjani, pengine hii inachangiwa na kukaa muda mrefu ndani ya timu.

Licha ya kuvuliwa unahodha mwanzoni mwa msimu na kupewa Method Mwanjali lakini bado alionekana kua mtu muhimu na sahihi pindi awapo uwanjani kwa kuwapa maelekezo wenzake pia kuwatuliza pindi timu inapokua imezidiwa.

Image result for Jonas Mkude images

Huyo ndie Jonas Gerald  Mkude Nahodha kwa wakati wake alieweza kuirudisha   Simbasc katika michuano ya Kimataifa kwa kuipa kombe la shirikisho mwaka jana jijini Dodoma.

Kesho ntakupitia apo Bokko Beach Veteran mazoezini nichukue viatu namimi nianze kua kama wewe.

Sambaza....