Roma vs SPAL 2013
Roma kushinda.
Sababu.
Form ya sasa kwa hizi timu. Mechi tano zilizopita, Roma ameshinda mechi 4 na kufungwa mechi 1. Wakati SPAL 2013 katika mechi tano zilizopita imeshinda mechi 1 na kufungwa mechi 4.
Katika mechi tano zilizopita kati ya Roma na SPAL 2013, Roma hawajafungwa na SPAL 2013 katika mechi hizo tano zilizopita ambapo Roma ameifunga SPAL 2013 Mara 4 na kutoka sare 1.
SPAL 2013 inahistoria mbaya kwenye mechi za ugenini dhidi ya Roma ambapo katika mechi 16 zilizopita ambazo wamecheza ugenini dhidi ya Roma wameshinda mechi moja, wakatoka sare mechi sita na kufungwa mechi Tisa.
JUVENTUS vs GENOA.
Juventus kushinda.
Sababu:
Tangu waanze msimu huu, katika mechi nane zote za Seria A msimu huu Juventus wameshinda mechi zote nane. Hii inaonesha wako kwenye kiwango kizuri sana tangu ligi ianze.
Katika mechi kumi zilizopita zilizowakutanisha Juventus na Genoa, Juventus imeshinda mechi nane na kufungwa mechi 2.
Na katika mechi tano zilizopita ambazo Juventus waliikaribisha Genoa katika uwanja wake wa nyumbani, Juventus wameshinda mechi zote tano tena bila kuruhusu hata goli moja. Mara ya mwisho kwa Juventus kufungwa na Genoa ilikuwa mwaka 1991.
Manchester City vs Burnley.
Manchester City kushinda
Sababu
Manchester City haijapoteza mechi yoyote katika mechi tano zilizopita dhidi ya Burnley. Na Burnley hawajawahi kushinda katika mechi 14 zilizopita nyumbani kwa Manchester City.
Manchester City hawajawahi kufungwa katika mechi 33 zilizopita za ligi kuu ya England zilizochezwa muda wa saa kumi na moja alfajiri.
PSG vs Amiens.
PSG Kushinda.
Sababu
Paris Saint Germain haijawahi kupoteza katika mechi tatu zilizopita dhidi Amiens ambapo imeshinda mechi mbili na kutoka sare katika mchezo mmoja dhidi ya Amiens.
Kiwango cha sasa za hizi timu.
Katika mechi tano zilizopita, PSG imeshinda mechi 5 zote . Wakati Amiens katika mechi tano zilizopita wameshinda mechi mbili na kushindwa mechi tatu.
Bayer Leverkusen vs Hannover 96.
Bayer Leverkusen kushinda.
Sababu
Katika mechi sita zilizowakutanisha Bayer Leverkusen na Hannover 96, Bayer Leverkusen wameshinda mechi sita(6) na kutoka sare mechi moja.
Viwango vya sasa vya timu husika.
Katika mechi tano zilizopita Bayer Leverkusen imeshinda mechi 3, ikatoka sare mchezo mmoja na kufungwa mchezo mmoja. Wakati Hannover 96 imefungwa mechi 4 na kushinda mechi moja katika michezo mitano iliyopita.
Mara ya mwisho kwa Bayer Leverkusen kufungwa na Hannover 96 ilikuwa mwaka 2012. Mpaka sasa wameenda mechi 9 mfululizo bila kufungwa na Hannover 96.
Katika mechi 10 zilizopita walizocheza nyumbani dhidi ya Hannover 96, Bayer Leverkusen haijawahi kufungwa katika mechi hizo 10 zilizopita walizocheza nyumbani dhidi ya Hannover 96.
Bayer Leverkusen imeshinda 83% za mechi ambazo wamecheza nyumbani dhidi ya Hannover 96. Ikiwa ni wastani mzuri kuzidi timu yoyote kwa sasa kwenye Bundesliga.