Kumekuwa na taarifa za ndani kuwa Mtendaji mkuu wa Simba , Magori kuondoka Simba na kuna habari za mtendaji mpya kutoka nje ya nchi kuchukua nafasi yake.
Mwenyekiti wa klabu ya Simba amedai kuwa mkataba wa Magori umeisha lakini bado anaendelea kuhudumu ndani ya klabu hiyo.
“Ni kweli alikuwa na mkataba wa miezi 6 na mkataba wake umeisha kwa sasa. Ila bado anaendelea kuwa mtendaji wa Simba mpaka pale tutakapotangaza jambo jingine”- alidai mwenyekiti huyo wa Simba, Sued Kwambi.