Pamoja na kwamba Kocha mkuu wa Yanga kuonekana kusikitishwa na kiwango cha waamuzi katika mchezo wa jana dhidi ya Mbeya City ambao ilimalizika kwa sare ya 1-1 kocha huyo amegusia kuhusu safu mbovu ya ushambuliaji.
Kocha huyo aliulizwa kwanini timu yake inapata mipira michache kwenye eneo la mwisho (final third ) na safu yake ya ushambuliaji kuonekana butu, Kocha huyo alidai kuwa yeye kazi yake ni kufundisha jinsi ya mpira kufika sehemu na siyo kufunga.
“Mimi mchezaji niliyemsajili ni Bernard Morrison, kuhusu washambuliaji wengine jaribuni kuwauliza uongozi wa benchi la ufundi lililopita.
“Kazi yangu Mimi ni kuhakikisha mpira umefika hapa , umefika pale . Mpira ukifika karibu na goli ni kazi ya mchezaji kuamua kushuti au kupiga pasi “. alisema kocha huyo .
Kuhusu kupigiwa kelele ya kuwachezesha baadhi ya wachezaji kocha huyo amedai kuwa amejaribu kufanya hivo kwa mmoja wao ambaye ni Tariq na anawaachia watu waone.
“Nimemjaribu Tariq , Mimi sitaki kuongelea kitu chochote nawaachia mashabiki wamuone kama anafaa , Mimi nawapongeza wachezaji wangu kwa kupigana kwa nguvu zote “- alimalizia kocha huyo wa Yanga