Santiago Bernabeu, uwanja ambao ulikuwa na nyasi ambazo zilichagua ng’ombe wa nyumbani kupata malisho.
Kutoka na ubabe wa ng’ombe ngeni tulitegemea kwa kiasi kikubwa ungemfanya amzidi ng’ombe mwenyeji
Magoli matatu yalitosha kumpa pumzi ndefu mwenyeji, pumzi ambayo anaenda nayo ƙkatika uwanja wa Parc des Princes.
Uwanja ambao umekuwa siyo salama kwa kila timu inayokanyaga kucheza na PSG.
Uwanja ambao msimu huu PSG wamefungwa goli moja katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya.
3-0, 5-0 na 7-1 ndiyo matokeo ya kikatili ambayo yaliwahi kufanywa na PSG dhidi ya timu ambazo zilikanyaga nyasi za Parc des Princes msimu huu.
Magoli 15 katika uwanja wao wa nyumbani na wanahitaji ushindi wa magoli 2-0.
Kitu ambacho kinaonekana chepesi kwao kwa sababu na historia kuonekana kuwabeba wao.
Msimu huu wamefanikiwa kufunga magoli kuanzia mawili katika michuano ya klabu bingwa ulaya wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani.
Mwaka 2014 walifanikiwa kuifunga Chelsea magoli 3-1 katika uwanja huo huo, na msimu wa mwaka jana walifanikiwa kuifunga Barcelona magoli 4-0 katika uwanja wao wa nyumbani.
Kitu hiki ni kielelezo tosha kuwa PSG huwa wanakuwa mbogo kipindi wanapokuwa wamekanyaga nyasi za uwanja wao.
Viingilio vya mashabiki wao huwa wanavionea huruma, ni mara chache sana huwauzunisha mashabiki wao katika uwanja wao wa nyumbani.
Katika mechi 19 za msimu huu ambazo PSG kacheza katika uwanja wa nyumbani kafanikiwa kufunga magoli 76, ikiwa ni wastani wa kufunga magoli 4 kila mechi.
Safu yao ya ushambuliaji huwa haishibi haraka inapokuwa nyumbani.
Udhaifu wa beki ya Real Madrid inaweza ikawa faida kwa PSG?
Varane na Ramos wamekuwa na kiwango kisichokuwa kizuri sana ukilinganisha na msimu jana, safu yao ya ulinzi imekuwa ikiruhusu kufungwa magoli magoli mengi msimu huu.
Mfano katika ligi kuu ya Hispania pekee , wameruhusu kufungwa magoli 29 msimu huu. Na katika michezo 15 iliyopita wamefanikiwa kutofungwa goli katika michezo miwili pekee.
Michezo mitano iliyopita hawajafanikiwa kupata clean sheet (kutoruhusu kufungwa goli)
Hii ni kutokana na kiwango cha safu ya ulinzi ya PSG imekuwa siyo imara sana. Ramos na Varane wamepungukiwa kasi na umakini , Marcelo amekuwa anaisaidia sana timu inapokuwa inashambulia lakini inapokuwa inashambuliwa imekuwa ngumu kwake.
Hivo safu ya ulinzi ya ƊReal Madrid isipojirekebisha mbele ya PSG ambayo ina takwimu nzuri za magoli katika uwanja wao wa nyumbani, tunaweza kushuhudia PSG akipindua matokeo.
Pengo la Neymar linaweza kuwateteresha PSG?
Anaikosa mechi ya leo, mchezaji ambaye amehusika katika magoli mengi ya PSG msimu huu.
Leo hii hayupo, ni namna gani PSG wanaweza kucheza bila yeye na kufanikiwa kupata ushindi siku ya leo?
Kwanza kuna faida kwa kutokuwepo kwa Neymar kwenye mechi hii, moja ya faida ni PSG kuwa na njia nyingi za wao kupatia magoli.
Asilimia kubwa ya mashambulizi ya PSG hupitia upande ambao Neymar huwa anakuwepo, sasa leo hayupo kitu ambacho kitamsaidia PSG ni yeye kupata njia nyingi za kupitishia mashambulizi yao.
Ni mchezaji yupi anafaa kucheza sehemu ya Neymar?
Angel Di Maria, ni mmoja ya wachezaji ambao wanaweza wakawa hawana sanaa kubwa kama ya Neymar lakini wakawa na madhara ya moja kwa moja.
Ana magoli 17 mpaka sasa katika mashindano haya ya ligi ya mabingwa barani ulaya.
Hii inatosha kuonesha ana uzoefu ambao unaweza kuwasaidia PSG katika mechi hii
Kipi kitakuwa msaada kwa Real Madrid ili waweze kufanikiwa kuvuka hatua hii?
Moja ya matatizo makubwa ambayo PSG imekuwa ikikumbana nayo hasa hasa inapokutana na timu kubwa ni eneo lao la kiungo cha kuzuia kutokuwa imara.
Thiago Motta amekuwa ni mtu muhimu eneo hili lakini anapokosekana kwenye mechi kubwa PSG huonekana inayumba, leo hii wanamkosa tena Thiago Motta, kwa hiyo hii inaweza ikawa faida kwa kiasi kikubwa kwa Real Madrid.
Kiungo cha kuzuia kinapokuwa hakiko imara kina nafasi kubwa sana ya kuifanya safu ya ulinzi kupokea mashambulizi mengi, hivo kama Toni Kroos na Luka Modric wakiweka presha eneo la kiungo kutakuwa na nafasi kubwa kwa Real Madrid kupita hatua hii na kwenda hatua nyingine