Sambaza....

Msimu wa tatu wa michuano ya SportPesa unatarajiwa kuhitimishwa Jumapili hii kwa michezo miwili, mmoja ukiwa ule wa kutafuta mshindwa wa nafasi ya tatu na mchezo wa fainali.

Kama ilivyokuwa kwa msimu wa kwanza ambapo timu kutoka Kenya Gor Mahia na AFC Leopards walicheza kwenye ardhi ya Tanzania kutafuta mshindi ndivyo itakavyokuwa jumapili hii ambapo Kariobangi Sharks watakuwa na kibarua kizito watakapocheza na Bandari FC.

Safari za timu zote mbili:

Bandari kutoka Mombasa nchini Kenya wao walianza mchezo wa kwanza kwa kuwaondoa Singida United kwa bao 1-0 kabla ya kuwaondoa mabingwa Tanzania Simba SC kwenye mchezo wa nusu fainali kwa mabao 2-1.

Kariobangi Sharks wao walianza michuano hii kwa ushindi mjarabu dhidi ya Young Africans, ushindi wa mabao 3-2 kabla ya kuwaondoa Wabishi, Mbao FC kwa mikwaju ya penati 6-5 baada ya sare ya 0-0 katika muda wa kawaida.

Mchezo huu wa fainali ambao utatafuta timu itakayokwenda kukutana na Everton ya nchini Uingereza, utaanza majira ya saa 10:00 jioni ambapo mbali na kukutana na Everton lakini pia mshindi atajinyakulia Shilingi Millioni 60.

Watanzania kuwania nafasi ya Tatau:

Aidha mapema kabisa kutakuwa na mchezo wa kuisaka nafasi ya tatu ambapo Simba SC watacheza na Mbao FC, mchezo ambao unatarajiwa kuanza majira ya saa nane mchana.

Utakuwa ni kama mchezo wa kisasi kwa Simba SC kwani katika mchezo wa ligi uliozikutanisha timu hizo kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, Mbao waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Sambaza....