Endelea kusoma sehemu hii ya nne ya mfululizo wa makala ya ‘Mh. Mwakyembe, Winners take control’
Baada ya somo lile la Wajerumani mwaka 2009 na 2010 Uingereza ilirudi kwenye msingi na kuachana na vita walivyovishindwa dhidi ya wachezaji wa kigeni kwa kuzifumua shule zao za mpira wa miguu za vilabu, hata taasisi nyingine kwa kutengeneza mitaala mipya, anaandika Cristina Esguerrawa DW.com. Baada ya miongo kadhaa ya kukatishwa tamaa hatimae Uingereza kupitia mapinduzi makubwa katika programu za soka lake la vijana wametwaa ubingwa wa Dunia kwa mara ya kwanza na ubingwa wa Ulaya kwa vijana wake wa miaka chini ya miaka 20 na 19; huku vijana hao wa chini ya miaka 20 wakiwashangaza wengi wakitwaa ubingwa huo wa Dunia bila kupoteza mechi hata moja, mafanikio ya waingereza hayakuishia kwa vijana hao wa chini ya miaka 20 na 19 bali yaliendelea kwa vijana wake wengine wa chini ya miaka 17 na wale wa chini ya miaka 21 wakifika fainali na nusu fainali kwa mashindano ya ngazi za vijana ya Ulaya.
Mafanikio hayo hayakuja tu kama ndoto bali ni kufatia mpango wa muda mrefu wa kuwaendeleza wachezaji wa Kiingereza kuanzia mwaka 2012 ikiwa na dhamira ya kutwaa Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar, na matokeo ya mwaka 2018 ya Kombe la Dunia na yale ya Euro League kwa timu ya Taifa ya Uingereza kufika hatua za Nusu Fainali kwa mashindano yote mawili unaweza kuona namna wameanza kupata uelekeo mzuri; kufatia mpango madhubuti wa FA kutengeneza mpira wa taswira yao (England new DNA)FA ilikuja na Alama kuu 5 kuwezesha mpango huo;
- Sisi ni nani? Lengo kuu ni kuwafanya vijana wa kiingereza kuwa na hamu ya kuchezea timu yao ya taifa, wakisherehekea kila hadithi ya mmoja wapo katika mafanikio yake na kuwafanua kuwa kitu kimoja na kuwaleta pamoja kama timu anasema Mkuu wa Makocha na Muendeleza vipaji wa vijana; Bwana Matt Crocker kutoka FA.
- Vipi tunacheza?/ Namna gani wacheze? Lengo hasa kutengeneza mfumo ambao timu zote za taifa zitacheza kuanzia ile ya miaka chini ya 15 hadi timu ya wakubwa
- Wachezaji wa wakati ujao; lengo hasa kuangalia wachezaji wa wakati ujao ambao tabia zao, namna wanavyoishi na hata wanavyocheza wataendana na mahitaji ya mtindo wa timu yao ya taifa ya wakubwa.
- Namna ya kufundisha; kutengeza mtaala ambao utakuwa endelevu na wenye kudumu ambao utatumika katika kufundisha vijana wote nchini Uingereza katika filosofia moja.
- Jinsi ya kuunga mkono; kuunganisha nguvu kwa pamoja katika kudumisha huduma na misaada thabiti ya kisayansi, michezo, uchambuzi wa matibabu na ukuzaji wa saikolojia ya vijana wakielekea kuwa wachezaji wakubwa, alisema Bwana Crocker
Kuelekea kwenye Ujenzi wa timu mpya za taifa za Uingereza FA walikuja na kiwanja kikubwa cha mazoezi cha kuitwa St. Georges Park ambapo una viwanja 13 tofauti kiwanja kimoja kikiwa kimejengwa katika mfanano wa Uwanja mkuu wa taifa hilo Uwanja wa Wembley, pamoja na uwanja huo pia kuna Gym za kisasa pamoja na vifaa vya michezo vya kisayansi ikijumuisha Hotel ya kifahari ya ya Hilton, ambapo timu zote za Taifa za nchi hiyo huweka kambi kujiandaa na mechi zake za mashindano hata za kirafiki, uwanja huo wa mazoezi ulizinduliwa rasmi mwaka 2012 ikiwa ni Alama ya Mipango mipya ya Taifa hilo kuelekea kwenye kulitawala soka la ulimwengu.
Bwana Crocker anasema mpango huo wa St. Georges Park ni sawa na ule wa Ufaransa wa Mwaka 1988 walipotengeneza kituo cha michezo cha Clairefontaine na miaka 10 baadae 1998 Ufaransa ilitwaa Kombe la Dunia nchini kwao kwa kuwatumia wachezaji waliotengenezwa kukidhi mahitaji yao, akiendelea Bwana Crocker alisema wanajifunza kutoka kwa mataifa mengine kama Waholanzi, Wahispania, Wafaransa, na Wajerumani kwa kuwatumia wataalam wao lakini hawajajifungia kutokujifunza kutoka kwa vyama vya michezo mingine kama Chama cha waendesha Baiskeli cha Uingereza, Chama cha Mpira wa Magongo cha Uingereza ama chama cha mpira wa Miguu cha Wamarekani (American Football)
Hii inawafanya vijana kushindana vyema na hata kushinda makombe kitu ambacho kinawafanya hata wakienda kuwa wachezaji wa timu ya wakubwa watabaki na tabia ya kujua kuwa wao ni washindi kwasababu wakiwa pamoja katika umri fulani walishinda ubingwa aidha wa dunia ama wa ulaya; kitu ambacho hapo kabla hawakukipata kwenye ngazi ya vilabu kwa kuwa kwa asilimia 69 Vilabu vya ligi kuu viliwategemea wachezaji wageni na wao kuishia kwenda kucheza kwenye timu za madaraja ya chini hapo kabla
Soma mfululizo wake kesho asubuhi…...
Jadili na Mwandishi wa makala hii katika sehemu ya maoni….