Sambaza....

Endelea kusoma sehemu hii ya tatu ya mfululizo wa makala ya ‘Mh. Mwakyembe, Winners take control’

Hizi ni baadhi ya sababu za waingereza baada ya timu yao ya taifa kutolewa kwenye hatua za mwanzoni za Kombe la Dunia kabla ya kuja na sababu ya wachezaji wa kigeni, Kombe la Dunia 1970 Kipa wa Uingereza wa wakati huo Gordon Banks alipata maradhi ya tumbo na hivyo kushindwa kucheza mechi ya robo fainali dhidi ya Ujerumani Magharibi, mechi ambayo ilibidi acheze Peter Bonetti ambae ilionekana amefungwa magoli ya kizembe matatu na kuanzia pale alikuwa akiimbwa “Umetupotezea Kombe la Dunia” fikiria hiyo ilikuwa ni mechi ya robo fainali maana yake kulikuwa na mechi mbili mbele kabla ya kutwaa Ubingwa wa Dunia kwenye mechi ya fainali.

Kombe la Dunia 1998 mbuzi wa kafara alikuwa David Beckham, Gazeti moja maarufu liliandikaNi Makosa ya mpuuzi mmoja mwaka 1950 na mwaka 1958 Mbuzi wa kafala walikuwa Kocha wa na Nahodha wa timu, lakini pia Mashabiki wa Mexico kwa kuchelewesha mipira kurudi uwanjani, 1986 Refarii na wasaidizi wake hawakuona goli la mkono la Maradona, lakini mashabiki wa Brazil mwaka 1950 na wale wa Mexico mwaka 1970 walikuwa wanachelewesha mpira wakati waingereza wapo nyuma, Mwaka 2006 kwenye Kombe la Dunia pale Ujerumani safafri hii Mbuzi wa Kafala alikuwa ni Cristiano Ronaldo aliyetajwa kama mtu aliyetumia nguvu kubwa kumshawishi Refarii kumpa kadi nyekundu Wayne Rooney baada ya mshambuliaji huyo kumkanyaga kwa makusudi beki wa Timu ya taifa la Ureno Ricardo Calvalho. Kombe la Dunia 2010 ni Manuel Neuer kutokuwa mkweli kukubali kwamba mpira uliopigwa na Frank Lampard ulivuka mstari. Kipigo pekee ambacho waingereza walikubaliana nacho ni kile tu walichoata dhidi ya Brazil kombe la Dunia mwaka 2002 kutoka kwa Timu ya Taifa ya Brazil kwa kusema walistahili kufungwa na katika kumaanisha kwamba walikuwa sahihi watakwambia Brazil walichukua Ubingwa hii wakidai kama wasingekutana na wabrazil pengine wangefika hadi fainali na pengine kutwaa ubingwa, inachekesha au vipi?

katika jambo la kushangaza marazote timu ya taifa ya Uingereza inapokuwa inaelekea kwenye mashindano makubwa mara zote wamekuwa wakijinasibu kubeba kombe kwa kuandikwa na kupambwa vyema na vyombo vyao vya habari, ni mwaka juzi tu hapa walikuja na Kauli mbiu “Is Coming Home” lakini mwisho wa mashindano wanarudi kwenye maisha yao ya kawaida na kutafuta mtu wa kumgeuza mbuzi wa kafala, kama ukiwa mtu wa hesabu kidogo tu utaona ilikuwa ni jambo la kipuuzi kufikiria kuwa Uingereza itatwaa kombe lijalo la Dunia hata ulaya kwa sera zao za soka la vijana hata namna ya kuwaandaa na kuwaendeleza wanasoka wao!

Alipoulizwa Sven Goran Erickson aliyekuwa Kocha wa timu ya taifa ya uingereza kwenye Kombe la Dunia mwaka 2002 na Kombe la Ulaya mwaka 2004 kuhusu kufanya vibaya kwa Uingereza alisema, “wachezaji wangu walikuwa wamechoka sana uchovu ulioletwa baada ya msimu mgumu sana”alipoulizwa kama hiyo ndilikuwa sababu pekee Eriksson alijibu “Naweza kusema hivyo” akaendelea kuelezea kama haupo na utimamu wa kutosha ni ngumu sana kushinda mechi akakumbushia kwamba walipokuwa kwenye Kombe la Dunia Korea na Japan mwaka 2002 hawakuweza kufunga goli lolote katika kipindi cha pili katika mechi zote walizocheza; Eriksson alijitahidi kuzungumzia sababu za kiutaalamu kutoka kwenye kundi la wachezaji aliokuwa nao kipindi anaifundisha Uingereza na hakujaribu kutupia lawama wachezaji wa kigeni kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Tanzania tumekuwa wahanga wa tabia hii ya Waingereza na mbaya zaidi sisi tumeamua kuibeba kwenye mioyo yetu, tumekuwa wahanga kwa kuiga kila kitu toka kwa wakoloni wetu hawa waliotuchukua mikononi mwa Wajerumani, tunaiga namna wanavyoandika habari za uongo kwenye magazeti yao, tunaiga namna wanavyolaumu watu wengine kwa kushindwa kwao wao wenyewe, tumekuwa wazuri sana wa mipango ya kwenye makaratasi utekelezaji ukiwa sifuri, tumekuwa mabingwa wa kutafuta nani wa kumtupia lawama badala ya kujiangalia sisi wenyewe, jambo baya zaidi kwetu ni kwamba wakati Waingereza wakiacha kulaumu uwepo wa wachezaji wa kigeni wenye vipaji vya hali ya juu kwenye ligi yao kama Kevin de Bruyne, Mohamed Salah, Sadio Mane, na hata kuendelea kuruhusu wengine kuingia kama Bruno Fernandes kwamba ndio kufanya kwao vibaya sisi ndio tunapiga makasia kuwaondosha akina Clatous Chota Chama, kwamba hatutaki kuwaona akina Yakoub Mohammed kwamba eti akina Obrey Chirwa wanasababisha vipaji vya wachezaji wetu kufa hivyo kufanya vibaya kimataifa, inachekesha hii kama sio kuhuzunisha!

Chama, Simba SC (Kushoto) na Adeyum, Yanga Sc (Kulia)

Wakati Uingereza ikiamua kuwekeza kweli kweli kwenye Soka na kuacha kupiga porojo urojo sisi ndio tunaona zitatusaidia jambo la ajabu na kushangaza, wazungu walipata kusema “Numbers don’t lie, people do” sasa sikia hii; Mwaka 2009 Uingereza ilifanikiwa kucheza fainali ya Kombe la Ulaya dhidi Ujerumani kwenye mashindano ya timu za taifa za vijana chini ya miaka 21 na kufungwa goli 4 kwa sifuri, cha kushangaza kikosi kile cha waingereza cha vijana hakikutoa mchezaji hata mmoja kwenye kombe la dunia 2010 huku nusu ya vijana wale wa kijerumani waliocheza fainalia ya kombe la ulaya kwa vijana wa chini ya miaka 21 mwaka mmoja nyuma yaani mwaka 2009 walikuwa ni sehemu ya kikosi kilichowafunga tena waingereza magoli 4 kwa 1 nchini Afrika Kusini kwenye hatua ya 16 bora za Kombe la Dunia na miaka minne baadae mwaka 2014 ni Mchezaji mmoja tu James Milner ambae alikuwepo mwaka 2009 kwenye kikosi cha timu ya vijana ya Uingereza U21 iliyobugizwa goli 4 kwa 1 ndio alisafiri na timu ya wakubwa ya Uingereza kwenda Brazil kwenye kombe la Dunia ambalo timu ya taifa ya ujerumani iliyosheheni vijana ile timu Ujerumani U21 mabingwa wa Kombe la vijana la U21 wa Ulaya mwaka 2009 ndio kikosi kilichofanikiwa kutwaa kombe la Dunia nchini Brazil wakiifunga Argentina kwa goli la Mario Gotze katika kipindi cha pili cha dakika 30 za nyongeza, hii itoshe kutuonesha kwamba mpira hauendi bila kuwa na mipango madhubuti kumbuka Ligi kuu ya Ujerumani ina asilimia 15.1 ya wachezaji wazawa wanaoanza kwenye timu zake kwa utafiti wa CIES Football Observatory toka mwaka 2009 hadi 2017.


Soma mfululizo wake kesho asubuhi…...

Jadili na Mwandishi wa makala hii katika sehemu ya maoni….

Sambaza....