Tupo kati kati ya mazungumzo ya kundi sogozi “Whatsapp” mara Mkongwe mmoja wa kuitwa Jeremiah akatuma video, kwa kuwa video ile ilitumwa na Mkongwe sikutaka kuidharau nikaifungua kuitazama nilichokutana nacho ni mahojiano ya Mchezaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United FC na Arsenal Fc na Uingereza, Feyernood FC ya Uholanzi na Besiktas FC ya UturukiBwana Robin van Persie akihojiwa na kituo kimoja cha Redio akizungumzia “Tabia za watu washindi” baada ya kijana wake Shaqueel ambae anacheza katika timu ya vijana ya Feyenoord U14 kutochezeshwa katika mechi dhidi ya Ajax U14 na kijana yule kusema kuanza kutupa shutuma kwa watu wengine akisema….Kocha hampendi na lawama nyingine nyingi kwa wachezaji wenzie na hata wafanyakazi wa timu ile ya watoto ya Feyernood!
Van Persie akimjibu mtoto wake alisema …. I said to Shaqueel….
Shaqueel you sound like a loser, you know, if you talk like this in a way, you sound like you lost. You are blaming him, you are blaming her, you are blaming this, and you are blaming everything…. But I don’t hear one single thing about yourself, WINNERS THEY TALK CONTROLand they blame themselves and they look where they can improve.” ….. “You should ask yourself the question are you a loser or are you a winner?
Wiki hii mjadala uliopamba moto kwenye vyombo vya habari na hata mitandaoni ni kutupiwa lawama kwa wachezaji wa kigeni “Waliofurika kwenye Ligi kuu Tanzania Bara” kwamba “wanaua vipaji” ama wanawanyima wazawa nafasi ya kucheza hivyo inapaswa namba kupunguzwa kutoka ya sasa ya wachezaji 10 wa kigeni hadi kufikia wachezaji 5 ama wa 3.
Mjadala huu umepata wachangiaji wengi sana wanaopinga na wanaosapoti, nikatamani nami nitoe mawazo yangukatika hili huku nikiweka na mifano hai kabisa kupitia maandiko ya kisayansi yaliyowahi kuandikwa na wasomi na waandishi wengine ili tu ku cement hoja yangu napenda kutumia maneno yale yale kwamba WINNERS TAKE CONTROL kama Robin van Persie alivyochukua muda kumwambia kijana wake Shaqueel dakika chache baadae Mkongwe mwingine wa kuitwa Salugado akatuma video nyingine akiitag ile video ya Mkongwe Jeremiah hii sasa ikimuonesha mtoto mwenye umri wa miaka 13 wa kuitwa Shaqueel akifanya mazoezi kwa bidi nikaanza kutafakari juu ya Huu mjadala wa kupunguza wachezaji wa kigeni kwenye ligi yetu ya juu kuliko zote Ligi kuu Tanzania bara yenye Udhamini mnono wa Vodacom(T) Company Limited.
Kwanza niseme tu hili sio jambo jipya kutokea hapa nchini ilishawahi kusemwa hapo kabla kwamba wachezaji wa kigeni wanachangia Tanzania kutopata timu bora ya Taifa kwasababu wao ndio “wamejaa” kwenye ligi yetu kipindi hicho hakukuwa na ukomo wa wachezaji hivyo Shirikisho la Mpira wa Miguu TFF likaweka ukomo kuwa wachezaji 10, ligi ikachezwa lakini ikaonekana kuwa bado wachezaji 10 ni wengi wakapunguzwa hata kufikia wachezaji 5 ligi ikachezwa timu zikakosa kupata matokeo mazuri kimataifa hii ikapelekea Vilabu Viwili vikongwe Simba na Yanga kulalamikia wachezaji wazawa hawana uwezo wa kutosha kushindana na vilabu kama TP Mazembe iliyojaza wachezaji mahiri wa kigeni hivyo kulitaka Shirikisho la mpira wa Miguu (TFF) liongeze idadi ya ukomo TFF ikaridhia ikaruhusu ukomo wa wachezaji wa kigeni uwe wachezaji 7.
Villabu vyetu hivi viwili vikongwe vikasajili wachezaji hao saba; msimu ulipoishana kuja kutaka kuanza kwa msimu mpya klabu moja kongwe ikasajili wachezaji 9 wa kigeni TFF ilipotaka iwapunguze Klabu ile ikapeleka hoja za msingikwa TFF ambapo Shirikisho likashindwa kwenye hoja za Klabu ile kongwe, hivyo basi namba ya wachezaji wa kigeni ikarudi tena na kuwa 10 kama ndio ukomo hadi hivi sasa.
Soma mfululizo wake….