Mesut Ozil amekataa kuungana na wachezaji wenzake wa Arsenal kwa kukubali kukatwa mshahara kwa asilimia 12.5. Ozil ndie mchezaji anaelipwa kiasi kikubwa zaidi cha mshahara katika klabu ya Arsenal akiwa anapokea pauni 350,000 kwa wiki.
Ozil ameweka wazi kuwa anaweza kuwa tayari kuifanya baadaye lakini alitaka kuona athari kamili ya kifedha kutokana na ugonjwa wa corona na hakutaka kuharakisha uamuzi .
Mesuit Ozil ni mmoja wa wachezaji watatu kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal kutokubali kupunguziwa kiasi cha kulipwa. Ozil ameweka wazi kuwa anaheshimu wachezaji wengine na uamuzi wa kikundi, lakini amewasihi wamuheshimu pia.
Wakala wake, Dk Erkut Sogut alikataa kutoa maoni lakini hivi karibuni alisema kuwa wachezaji hawapaswi kukubali kupunguzwa kwa mshahara Sogut alisema mapema mwezi huu.
“Uhamisho ni chaguo lakini sio kukubali kukatwa leo wakati vilabu bado vinaweza kupata faida sawa na ya mwaka jana.”