Sambaza....

Inawezekana ndiyo wachezaji ambao wamegawana mashabiki katikati kwa kipindi cha muongo mmoja uliopita kama walivyogawa katikati tunzo ya Ballon D’or ndani ya miaka 10 iliyopita.

Miguu yao imetufurahisha sana, ikatuliza sana kwa furaha na huzuni na kupelekea upande mmoja wa mashabiki kuwa na chuki na Messi na upande mwingine kuwa na chuki na Cristiano Ronaldo tena chuki ambayo haina sababu.

Na hii ni kwa sababu huwezi kutaja mpira wa miguu kwa sasa bila kuwataja hawa watu wawili, binadamu ambao wamefanikiwa kuweka alama kwenye mchezo huu.

Pamoja na kuweka alama kwenye mchezo huu, kuna rekodi nyingi za kombe la dunia ambazo hawajawahi kuzifikia na kuna hatari za kutozifikia, rekodi hizo ni:

1:Mchezaji aliyeshinda Mara nyingi kombe la dunia. Rekodi hii inashikiliwa na mfalme wa Samba Pele ambaye amechukua mara tatu(3) katika michuano ya mwaka
1958,1962 1970.


2: Just Fontaine anaweza akabaki kama mchezaji wa ajabu kwenye michuano hii kwa sababu ya rekodi yake ya kufunga magoli 13 katika kombe la dunia la mwaka 1958 na kubaki kuwa mchezaji ambaye alifunga magoli mengi katika mchuano mmoja pekee akitumia michezo 6 tu kufunga magoli 13.


3: Kuna mengi sana ya kujivuia kwenye mpira sisi Waafrika kwenye mpira. Tuliwahi kujivunia George Weah leo hii tunajivunia Mohamed Salah na hii haitofanya tusimsahau Roger Miller ,mchezaji aliyefunga goli akiwa na umri mkubwa, 42 yes mwezi 1 na siku 8 katika kombe la dunia 1994. Mpaka sasa Cristiano Ronaldo ana miaka 33 na Messi ana miaka 30.


4: Miroslav Klose mchezaji mwenye roho halisi ya babu wa taifa la Ujerumani (Adolf Hitler), hakuwa na huruma na magolikipa kitu ambacho kimemsaidia kuwa mfungaji bora wa wakati wote wa michuano hii akiwa na magoli 16 aliyoyafunga katika michuano ya mwaka 2002, 2006, 2010 na 2014. Mpaka sasa Lionel Messi ana magoli matano (5) na Cristiano Ronaldo akiwa na magoli matatu(3).


5: Cafu anabaki kama beki bora wa kulia wa wakati wote, na ndiye mchezaji ambaye anashikiria kucheza mechi nyingi za fainali ya kombe la dunia. Alicheza mechi ya fainali mwaka 1994, 1998 na mwaka 2002.

Pele amechukua kombe hili mara tatu, lakini mechi ya fainali ya mwaka 1970 hakucheza tofauti na Cafu ambaye alicheza mechi tatu za Fainali ƴa kombe la dunia.

Sambaza....