Sambaza....

MLINZI wa kati wa Biashara United FC, Meshack Abel amesema licha ya ukosefu wa udhamini katika ligi kuu Tanzania Bara msimu huu, lakini bado anaamini ligi hiyo inaendelea kupiga hatua mbele.

Meshack mchezaji wa zamani wa Simba SC na timu ya Taifa ya Tanzania ( Taifa Stars) amejiunga na klabu hiyo changa katika ligi kuu kutoka mkoani Mara msimu huu na baada ya michezo saba beki huyo amenzungumza na mtandao huu mambo kadhaa.


Vipi unaonaonaje mwenendo wa ligi kuu kufikia raundi hii ya nane?

MESHACK ABEL

Kwa kweli ukiachana na kutokuwepo kwa wadhamini wakuu, lakni ligi pia ina ugumu wake kwasababu kila timu imekuwa ikijitahidi kadri inavyoweza.


Ukiwa na uzoefu wa kucheza klabtj kubwa Tanzania, kucdhezea timu iliyopanda ligi kuu kwa mara ya kwanza tena ligi yenyewe ikiwa haina udhamini kuna tofauti gani?

MESHACK ABEL

Tofauti ni kubwa, unajua unapocheza katika klabu kubwa na baadae ukatoka juu na kushuka chini tofauti inaanzia hapo, lakini kikubwa maandalizi ya klabu kubwa ni tofauti nay ale yanayofanywa na klabu ndogo, lakini mpira ni uleule tu.


Hamjaanza vizuri msimu, mechi saba, ushindi mmoja, sare tatu na vipigo vitatu, ukiitazama Biashara United unadhani mnaweza kunyanyuka?

MESHACK ABEL

Ndiyo, naamini tutaamka na kufanya vizuri kadri ligi inavyoendelea kuchanganya. Tuna timu nzuri na matokeo yetu yaliyopita tunayachukulia kama changamoto tu zilizopo katika soka-kuna kutoa sare, kushinda ama kupoteza mchezo.


Ukiachana na ukosefu wa udhamini katika ligi, nini ambacho kinaathiri ligi ?

MESHACK ABEL
Upande wangu nadhamini changamoto kubwa ni ukosefu wa udhamini katika ligi- hii ndiyo shida kubwa.


Katika michezo saba mliyokwisha cheza unazungumziaje uchezeshaj wa waamuzi?

MESHACK ABEL

Kumekuwa na mabadiliko kadhaa kutoka kwa waamuzi tofauti ya misimu ya nyuma, yapo makosa ya kibinadamu ambayo hutokea katika uchezeshaji wao lakini niwe mkweli, kwa upande wangu, waamuzi wamejitahidi kucheza vizuri hadi sasa labda hapo baadae.


Unazungumziaje upangaji wa ratiba?

MESHACK ABEL

Ni tatizo, ratiba imekuwa ikivurugwa sana. Tazama kuna timu nyingine zimecheza michezo michache sana tofauti na nyingine, tatizo linaanzia hapo. Wanatakiwa kutazama upya upangaji wao wa ratiba na kuacha kuipangua pangua.

Sambaza....