Meneja anaemsimamia mlinzi wa Coastal Union ya Tanga Mussa Kassa amesema mpaka sasa hakuna klabu yoyote ambayo wameshakubaliana kuhusu kumsajili Bakari Mwamunyeto.
Mwamunyeto amekua akihusishwa na vilabu vya Simba na Yanga katika kipindi hiki Ligi ikiwa imesimama huku kila mmoja akionekana kuiwinda saini ya mlinzi huyo wa timu ya Taifa anaefanya vizuri kwasasa.
Mussa Kassa “Hakuna klabu yoyote ambayo tumeshaafikiana kuhusu usajili wake (Bakari Nondo), kwanza usajili bado haujafunguliwa na ligi haijaisha hata Coastal tumekubaliana tusubiri kwanza mpaka msimu umalizike. Mwamunyeto ni mfanyakazi anaweza kuitumikia klabu yoyote ambayo tutaafikiana nayo.
Maana klabu zote zipo sawasawa (katika kuwania saini ya Mwamunyeto) isipokua kuna mambo madogo ambayo hayajawekwa sawa. Tutaangalia tuu klabu yoyote ambayo itaturidhisha, sisi klabu yoyote tuu sawa hatuwezi kusema sijui hatuwezi kucheza Yanga ama Simba.
Meneja huyo ambae kwasasa yupo nchini Italy pia amezungumzia thamani ya mchezaji wake na kusema mpira unachezwa hadharani kila mtu anaona uwezo wa Mwamunyeto.
“Ni mapema mno kuzungmzia thamani ya Mwamunyeto hayo ni mambo yetu sisi hatuwezi kusema thamani yake ni kiasi gani, lakini kila mtu anaona. Watu wengi wanapiga kelele lakini kitu cha kushangaza kuna wachezaji hapo wanakuja wanalipwa mishahara mikubwa na uwezo hawana.
Lakini hili la Mwamunyeto watu wanapiga kelele sijui milino mia au themanini. Watanzania lazima ifike wakati tuthamini vyakwetu, kama mchezaji mzawa yupo vizuri apewe haki yake tusifanye biashara kwa kujuana. Mpira hauna siri uwezo wa Bakari unaonekana uwanjani.” Mussa Kassa ambae pia ni mchezaji wa zamani wa Coastal Union.
Meneja Mussa Kassa amezungumza hayo katika kipindi cha michezo cha Efm.