Ruvu Shooting wakikutana na timu kubwa huwa wahahitaji kumiliki Mpira sana,na badala yake timu nzima hukuba vizuri eneo la kati, huziba mianya ya pasi mpenyezo na muda kwa timu pinzani kukaa na mpira na kufanya mashambuzi ya hatari na kushambulia kwa pamoja
Baada
- Simba ikiwa katika nafasi ya pili,ikijikusanyia jumla ya Alama 22 Huku Ruvu Shooting ikiwa katika nafasi ya kumi ikiwa na alama 15 pekee. Ni mechi ngumu ukizingatia, Ruvu Shooting tayari imeshazifunga timu zote zilizoshika nafasi nne za juu msimu uliopita isipokuwa Simba pekee. Yanga,Azam na KMC tayari Zimeshafungwa, anasubiriwa Simba tu.
Msimu uliopita,katika mechi ya raundi ya pili, Simba iliibuka na Ushindi wa goli 2-0, magoli yalifungwa na Beki Paul Bukaba na Mshambuliaji hatari Meddie Kagere. Presha ya mchezo huu ni kubwa ukizingatia, Kwa upande wa Simba kumekuwa na minong’ono ya kufukuzwa kwa kocha Patrick Aussems pia mechi hii ndio itakuwa mechi ya mwisho kwa Simba hadi tarehe 4, Januari watakapokutana na Mtani wake Young Africans.
Ili kujiandalia mazingira mazuri katika mchezo ujao dhidi ya Yanga, Simba ina presha kubwa ya kushinda mechi hii. Kandanda inatarajia mechi safi na ya kuvutia uzingatia aina ya soka timu zote mbili zinzolicheza.
RUVU SHOOTING.
Ruvu Shooting wakikutana na timu kubwa huwa wahahitaji kumiliki Mpira sana,na badala yake timu nzima hukuba vizuri eneo la kati, huziba mianya ya pasi mpenyezo na muda kwa timu pinzani kukaa na mpira na kufanya mashambuzi ya hatari na kushambulia kwa pamoja. Silaha kubwa ya Ruvu Shooting ni kushambulia kupitia pembeni, na kupiga mshuti kupitia katikati.
Pia wana golikipa mzuri ambaye kiukweli msimu huu amekuwa msaada sana kwa Ruvu shooting.
SIMBA SC.
Kama ilivyo kawaida yao, Simba humiliki mpira na kutengeneza nafasi kutumia pande zote za uwanja. Inategemeana na Kocha Aussems lakini kama ataanza na mawinga kama Hassani Dilunga na Deo Kanda huku kushoto kwao akaanza Mshambuliaji Miraji Athumani na Meddie Kagere Simba inaweza ikawa hatari zaidi kwa Ruvu Shooting.
Simba inaingia katika mchezo huu kwanza ikiwaza kukaa kileleni pili ni kupunguza presha kutokana na minong’ono ya hivi karibuni.
Je leo itakuwaje, baki na Mtandao wako wa Kandanda kwa habari na matokeo papo hapo.
Uwanja
Uhuru Stadium |
---|
Taarifa
Tarehe | Muda | Ligi | Msimu | Mwisho |
---|---|---|---|---|
23/11/2019 | 4:00 pm | TPL | 2019-2020 | 90' |