1: March 4/2020
Azam FC 2- 3 Simba
Wakati Simba anacheza mechi hii , mechi iliyokuwa inafuata ni mechi kati ya wageni wao wa jadi Yanga . Kuna vitu viwili ambavyo vilikuwa vinawapa wakati mgumu .
Mechi dhidi ya Azam FC ilikuwa muhimu , na Azam FC walikuwa wapinzani wa Simba katika kugombani ubingwa, Kwa hiyo kitu cha kwanza ambacho Simba walikuwa wanakiwaza ni namna ya kutopoteza alama yoyote mbele ya mpinzani wake wa ubingwa ambaye ni Azam FC.
Kitu cha pili ni mechi ya watani wao wa jadi , ni mechi yenye presha kubwa . Unatoka kucheza na Azam FC mechi inayofuata ni dhidi ya Yanga. Swali kubwa ni namna ambavyo wao wangeweza kushinda mechi dhidi ya Azam FC huku wakiwa na presha ya homa ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi lakini kwa bahati nzuri Simba hawakupoteza alama dhidi ya wapinzani wao wa ubingwa Azam FC.
2: February 2/2020
Simba 1- 0 Kagera Sugar
Msimu jana Kagera Sugar walikuwa na msimu mbaya, walikaa na kujirekebisha vizuri kwa ajili ya msimu huu . Walifanikiwa kufanya vyema msimu huu na walionesha ushindani msimu huu mpaka sasa hivi ni moja ya timu zinazofanya vyema.
Moja ya mechi ambayo Kagera Sugar walitoa ushindani mkubwa ni mechi hii iliyochezwa uwanja wa Taifa dhidi ya Simba , Simba walikuwa wanapresha ya kupoteza alama kwenye mchezo huu kwa bahati nzuri Simba walifanikiwa kutopeza alama kwenye mechi hii.
3: February 15/2020
Lipuli FC 0- 1 Simba
Lipuli FC kwenye mechi hii hawakutaka kuwa wanyonge . Pamoja na ubora wa Simba lakini Lipuli FC walionesha uwezo mkubwa sana kwenye hii mechi . Uwezo ambao ulitishia kwa Simba kupoteza alama lakini kwa bahati nzuri Simba walishinda goli moja kwa bila na kuepukana na kutopoteza alama kwenye mchezo huu.
4: February 4/2020
Simba 2-1 JKT Tanzania
Walicheza mechi mbili mfululizo . Mechi ambazo zilikuwa zina ushindani mkubwa , mechi ya kwanza ilikuwa hii ambayo ilimalizika kwa Simba kushinda goli 2-1 dhidi ya JKT Tanzania. Simba hawakupoteza alama kwenye mechi hii ngumu , lakini baada ya siku tatu walikutana tena na JKT Tanzania kushinda 1-0 dhidi ya Simba.
5: January 29/ 2020
Simba 3-2 Namungo
Namungo FC wamepanda daraja msimu huu lakini wameonesha uwezo mkubwa , uwezo ambao umewawezesha wao kushindana mara kwa mara kwenye nafasi tatu za juu ligi kuu .
Simba walikutana na ushindani mkubwa kutoka kwa Namungo FC , ushindani ambao uliofia uwezekano wa Simba kupata alama kwenye mchezo huu lakini Simba walifanikiwa kutopeteza alama kwenye mchezo huu pia .
6: January 01/2019
Mbao 1-2 Simba
Simba walisafiri Mwanza kwenda kucheza na Alliance FC mechi ambayo wakishinda goli 4-1. Pia walikuwa na mechi dhidi ya Mbao FC , mechi ambayo haikuwa nyepesi kama dhidi ya Alliance FC, Mbao FC walitoa ushindani Lakini Simba walifanikiwa kutopeteza alama pia.
7: December 28/2019
KMC FC 0-2 Simba
Kipi kinachokuja kichwani kwako ukikumbuka hii mechi ? Bila shaka ni maamuzi mabovu, maamuzi ambayo yalikuwa yanaonekana kuwabeba Simba , mechi hii Simba alikuwa na hatari kubwa ya kupoteza mechi.
8: October 27/2019
Singida 0-1 Simba
Pamoja na kwamba Singida FC kuonekana wachovu msimu huu lakini mechi hii waliwapa ugumu mkubwa Simba katika uwanja wao wa nyumbani wa Namfua mjini Singida. Lakini Simba walifanikiwa kutopeza alama pamoja na ugumu wa hii mechi.
9: September 13/2019
Simba 2-1 Mtibwa Sugar
Moja ya mechi ngumu za mwanzoni mwa ligi ni hii mechi kati ya Simba na Mtibwa Sugar . Mtibwa Sugar walionesha dhamira ya kupambana na Simba kwa kiwango kikubwa lakini Simba walipambana kutopoteza alama kwenye mchezo huu.