Sambaza....

Kylian Mbappe ameiambia Paris St-Germain kuwa hataongeza mkataba wake zaidi ya 2024, lakini anataka kusalia msimu ujao.

Hilo likitokea, mabingwa hao wa Ufaransa wana hatari ya kumpoteza kwa uhamisho wa bila malipo wa kiasi cha euro 180m (£165.7m) chini ya walivyomlipa mwaka wa 2017,  lakini ni idadi ndogo tu ya vilabu vinavyoweza kumudu.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, amefunga mabao 212 na kuchangia mabao 98 katika michezo 260 tangu ajiunge na PSG kutoka Monaco, awali kwa mkopo miaka sita iliyopita, akishinda mataji matano ya ligi kati ya mataji 13 ya nyumbani akiwa na klabu hiyo.

Kylian Mbappe na Neymar Junior.

Pia alikua mchezaji muhimu katika ushindi wa Kombe la Dunia la 2018 kwa Ufaransa na rekodi yake ya kimataifa ya mabao 38 katika mechi 68 inamweka nafasi ya tano kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote nchini mwake, mabao 15 nyuma ya Olivier Giroud anayeshikilia rekodi hiyo.

Mnamo Desemba, Mbappe alifunga hat-trick ya kwanza katika fainali ya Kombe la Dunia tangu 1966 lakini kupoteza kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Argentina kulimnyima ushindi mara mbili mfululio wa Kombe la Dunia akiwa na umri wa miaka 23.

Baada ya kufanya vyema na Ufaransa mara mbili katika fainali za kombe la Dunia 2018 na 2022 akishirikiana na kina Paul Pogba, Antonio Grieznman na Ngolo Kante pia fomu nzuri aliyonayo Ligue 1 imewafanya Real Madrid kutaka saini yake.

Kylian Mbappe.

Real walikuwa tayari kulipa euro 150m (£127m) kama ada ya kumsaini na mshahara wa euro 40m (£34m). Badala yake, Mbappe alichagua kukubali mkataba mpya na kusalia PSG, ingawa alisema ndoto ya kuichezea Real “haijaisha”.

Kuondoka kwa Mfaransa mwenzake na mshindi wa tuzo ya Ballon d’Or Karim Benzema kwenda Saudi Arabia kunamaanisha kuwa Real wako sokoni kutafuta mshambuliaji, huku Harry Kane wa Tottenham akidhaniwa kuwa kinara wa orodha yao ya wachezaji wanaosakwa.

Manchester United ni klabu nyingine kubwa ya Ulaya inayomwinda mshambuliaji huyu matata msimu huu wa joto na miongoni mwa vilabu vichache vya Ligi ya Premia vilivyo na uwezo wa kifedha kufadhili uhamisho.

Kylian Mbappe.

Bado kuna sintofahamu kuhusu umiliki wa baadaye wa klabu, hata hivyo, Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani na mzabuni mpinzani Sir Jim Ratcliffe wakisubiri kuona kama ofa zao za kununua klabu zitakubaliwa na familia ya Glazer.

Hata hivyo, habari za hali ya Mbappe huenda zikawashawishi United kumleta Mfaransa huyo Uingereza – na mmiliki yeyote mpya anayetarajiwa kupata fursa ya kuonyesha hisia zake za kwanza


Sambaza....