Sambaza....

Uwanja wa CCM Kirumba ulikuwa sehemu sahihi ya hukumu ya kesi kati ya Simba na Mbao.

Mbao walikuwa wanawakaribisha Simba ambayo ilitoka Mtwara ikiwa na alama moja baada ya kutoka suluhu na Ndanda FC.

Matokeo dhidi ya Ndanda FC yalionesha dhahiri Simba ilitumia nguvu kubwa kwenye mechi hiyo ya ugenini.

Tuliisubiri mechi ya Mwanza, mji ambao umekuwa mgumu sana kwa timu kubwa zinapokanyaga nyasi za CCM Kirumba.

Wachezaji wa Simba wakijiandaa kupiga faulo ambayo haikuzaa matunda

Mechi ya mwisho kwa Simba kukanyaga katika uwanja wa CCM Kirumba walitoka sare ya magoli 2-2.

Hivo kabla ilionesha hii mechi itakuwa ngumu na ukizingatia Mbao kaanza vizuri Ligi kuu msimu huu.

Kitu ambacho kiliipa nguvu Mbao kushinda mechi ya Leo kwa bao moja kwa bila.

Matokeo ambayo yanaipa nafasi Mbao kuongoza Ligi ikiwa na alama 10 mbele ya Yanga yenye alama 9, lakini Mbao wakiwa wamecheza mechi 5 na Yanga wakiwa na mechi 3.

Matokeo haya yatatoa nafasi kubwa kwa mashabiki wa Simba kuendelea na kilio cha Masoud Djuma kukabidhiwa timu. Wanamwamini sana!, wanampenda sana! na wanamwihitaji sana kwa sababu wanaamini katika mbinu zake kuna ushindi mkubwa wenye kuleta furaha.

Sambaza....