Dkt. Mshindo Msolla ameshaweka wazi kuwa mpaka kufikia mwakani (2020) mwezi wa tano (5) Yanga itakuwa kwenye mabadiliko ya uendeshaji wa klabu kutoka kwenye uendeshaji huu wa sasa mpaka kwenye uendeshaji wa kisasa.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo wa Yanga , Dkt. Mshindo Msolla mchakato umeanza mapema kwa sasa . Na Leo hii Afisa Mhamasishaji wa Yanga amedhibitisha hilo kuwa Yanga iko kwenye hatua za kubadili mfumo wa kuendesha timu.
“Kwa sasa hali yetu ya uchumi ni Mbaya , tunakosa hata hela ya usajili mpaka tunahisaniwa na watu. Hivo ili kuachana na hii hali lazima tuingie kwenye uendeshaji mzuri wa klabu , uendeshaji ambao utatuwezesha kulipa mishahara Kwa wachezaji , kupata pesa ya usajili kwa wachezaji”. Alisema Antonio Nugaz.
Alipoulizwa kuwa kama mabadiliko haya yamewalenga watu fulani , kama ambavyo Simba walifanya mabadiliko kwa kumlenga Mo kama kuja kuwa mwekezaji mkubwa ndani ya klabu , hivo Yanga na wao kuna tajiri ambaye wamemlenga ?, Antonio alisema kuna watu wengi wanaitaka Yanga.
“Kuna makampuni mengi yanaitaka Yanga mpaka sasa hivi , kuna kampuni kutoka falme za kiarabu linaitaka Yanga kwa sasa , pia timu yetu itakuwa timu ambayo inamilikiwa na matajiri watatu , siyo tajiri mmoja Siku akinuna mambo hayaendi”. Alimalizia kwa kusema hivo Afisa mhamasishaji huyo wa Yanga.
“Matajiri kutoka nchi za kifalme za kiarabu wametuma maombi ya kutaka kuwekeza Yanga sema kinachotia ugumu taratibu za nchi zinataka mwekezaji achukue asilimia 49 ya umiliki na wanachama wachukue asilimia 51 ya uwekezaji na wao hawa waarabu wanataka asilimia kubwa zaidi ya 49.” Alisema Afisa Mhamasishaji huyo wa Yanga alipokuwa anazungumza na kituo cha Wasafi FM. Kama Yanga ingefanikiwa kuchukuliwa na waarabu ingeungana na timu kama PSG inayomilikiwa na waarabu.