Aliyewahi kuwa kocha wa Rayon Sports na kocha msaidizi wa Simba Masoud Djuma amefukuzwa kazi katika timu ya As Kigali ya Rwanda.
Masoud Djuma ambaye amekaa kwa muda wa miezi 6 tu katika timu hiyo ya As Kigali ikiwa zimebaki siku 38 kabla ya mkataba wake kumalizika.
Masoud Djuma ameifanya As Kigali mpaka sasa hivi kushika nafasi ya 8 ikiwa na alama 30 katika michezo 23.
Masoud Djuma alikuwa kipenzi kikubwa sana katika kikosi cha Simba kabla ya kuachana na Simba kutokana na hali ya kutoelewana katika timu ya Simba.