Klabu ya Chelsea imewafungia mashabiki wake wanne kutokana
na tuhuma za ubaguzi wa rangi juu ya mshambuliaji wa Man City , Muingereza
Raheem Sterling katika mchezo uliochezwa siku ya jumamosi kati ya timu
hizo mbili .Klabu hiyo imetoa taarifa kwa umma inayosomeka hivi
Klabu ya Chelsea imebaini vitendo vya ubaguzi , nauchunguzi zaidi unaendelea lakini kama vitabainika dhahiri vitendo hivyo kuwani vya ubaguzi wa rangi kama klabuitachukua hatua kali zikiwemo za kuwafuta uanachama na kuunga mkono sheria zakiserikali kuchukua mkondo wake juu ya suala hilo
Raheem starling alifanyiwa vitendo hivyo kwa ushahidi uliosambaa mitandaoni kwa njia ya video inayowaonesha mashabiki wa Chelsea wakimzonga mshambuliaji huyo kwa maneno ya kibaguzi wakati terling akichukua mpira ili kupiga kona. Maneno hayo yalisikika hivi.. “black c****”.
Kwa sasa klabu ya Chelsea tayari imesha wasilisha ripoti yake juu ya mashabiki hao kwa polisi baada ya Sterling kuhojiwa jana asubuhi na kusema kuwa alisikia maneno hayo ya kibaguzi juu yake.
Kwa upande wao polisi, tayari wamesha muhoji shabiki mmoja
mwenye asili ya Afrika ambaye alikuwa pembeni wakati tukio lile linatokea na
amesema kuwa kwa upande wake hakusikia maneno yoyote ya kibaguzi kwa Sterling.