Moja ya vitu ambavyo mashabiki wa Yanga walikata tamaaa ni pale timu yao ilipopata suluhu dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Taifa.
Suluhu ambayo iliwafanya wapate alama mbili katika michezo miwili iliyopita tena katika uwanja wao wa nyumbani wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Taratibu mioyo yao imeanza kukata tamaa , inaona kabisa hakuna tumaini jingine ambalo wanalo kwa sasa baada ya kupata alama mbili ndani ya michezo miwili.
Hawaoni tena kama timu yao inaweza kupambania ubingwa kama ambavyo walivyokuwa wanaamini. Matokeo wanayoyapata na matokeo ambayo wanayapata Simba ni vitu ambavyo vinawafanya wakate tamaa .
Alipoulizwa Afisa Mhamasishaji wa Yanga kuhusu kitendo cha mashabiki wa Yanga kukata tamaa bwana Antonio Nugaz amedai kuwa hao ni mamluki.
“Yanga haina mashabiki wanaokata tamaa, hakuna kukata tamaa . Ukate tamaa kwa lipi ?, wanaokata tamaa ni mamluki na siyo mashabiki wa Yanga”- alidai Antonio Nugaz