Kocha wa timu ya Taifa ya Italia, Roberto Mancini amesema bado hajashawishika kumjumuisha mshambuliaji wa Marseille Mario Balotelli katika kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya michezo ya kufuzu kwenye fainali za Mataifa Ulaya mwaka 2020.
Mancini amesema licha ya Balotelli kuwa katika kiwango kizuri lakini bado hajawa sawa kifizikia kuweza kutumika kwenye michezo muhimu ya timu ya Taifa.
“Mario bado kidogo kuwa sawa kuichezea timu ya Taifa, amekuwa bora kifiziki ukifananisha na mwezi septemba lakini bado anahitaji kazi ya ziada, kwake nahitaji makubwa zaidi, karibu anakaribia umri wa miaka 29, ni muda wa kuwa kwenye kiwango chake, lakini kwa timu ya Taifa anatakiwa kuwa bora zaidi,” Mancini amesema.
Mbali na Mario ambaye toka ajiunge na Marseille amefunga mabao matano katika michezo saba aliyocheza lakini pia Mancini amemuacha nje Andrea Belotti mweye umri wa miaka 25 ambaye mpaka sasa amefunga mabao 10 ya ligi akiwa na Torino.
Hata hivyo katika kikosi hicho kitakachocheza mchezo wa kwanza Jumamosi dhidi ya Finland kabla ya baadae kuumana na Liechtenstein siku ya tarehe 26, kimemjuisha mchezaji mkongwe Fabo Quagliarella mwenye umri wa miaka 36 ambaye kwa sasa anaongoza kwa kuzifunia nyavu kwenye ligi kuu Seria akiwa na mabao 21 baada ya michezo 28.
Italy wanatafuta kurudisha tena heshima yao kwenye soka baada ya kushindwa kufudhu kwenye michuano ya kombe la Dunia mwaka jana, ikiwa ni kwa mara ya kwanza baada ya miaka 60.