Manchester City imeichapa Arsenal mabao 3-0, katika mchezo wa fainali ya kombe la ligi likijulikana kama Carabao Cup na kutawazwa kuwa mabingwa wa kombe hilo
Katika mchezo huo uliofanyika kunako uwanja wa Wembley na kuamuliwa na mwamuzi Craig Pawson Manchester City walipata bao la kwanza dakika ya 19 kupitia kwa Sergio Aguero likidumu hadi mapumziko
Kipindi cha pili timu zote ziliendelea kushambuliana kwa zamu, lakini walikua ni Manchester city waliofanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa beki wake Vicent Kompany kunako dakika ya 57
Wakati Arsenal wakiendelea kujiuliza namna ya kupata mabao ya kusawazisha, kiungo David Silva aliipatia City bao la 3 kunako dakika ya 65 na kufanya hadi dakika 90 za mchezo zinakamilika City wakiibuka washindi kwa mabao 3-0
Kwa ushindi huo, unaifanya klabu ya Manchester city, kuifikia rekodi ya Manchester United ya kushinda makombe mengi ya ligi sasa wakiwa wameshinda makombe 5 ya ligi
Hilo ni kombe la kwanza kwa kocha Pep Guardiola, tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Buyern Munich msimu mmoja uliopita, lakini pia likiwa ni kombe la 22, tangu alipoanza kufundisha mpira
Arsenal iliwakilishwa na David Ospina, Calum Chambers/Danny Welbeck dk 65, Shkodran Mustaf, Laurent Koscienly, Hector Bellerin, Granit Xhaka, Aron Ramsey/ Alex Iwob dk 73, Nacho Monreal/ Saad Kolasinac dk 26, Mesut O’zil, Jack Wilshere na Pierre Emerick Aubemeyang
Manchester city Craudio Bravo, Kyle Walker, Danilo, Vicent Kompany, Otamendi, David Silva, Fernandinho/ Bernardo Silva dk 52, Ilkay Guendogan, Leroy Sane/ Gabriel Jesus dk 77, Kelvin De Bruyne na Sergio Aguero/ Phil Foden dk 89