Sambaza....

Kuelekea mchezo wa kufuzu michuano ya Afcon mwaka 2023 kati ya mwenyeji Tanzanai dhidi ya Algeria kiongozi wa kamati ya hamasa ya Stars Haji Manara amezungumza na waandishi wa habari.

Mchezo huo utapigwa kesho jumatano June 8 saa moja kamili usiku katika dimba la Benjamin Mkapa. Haji Manara amesema wachezaji wetu wa Tanzania siku hizi wamekua na tabia ya kucheza vyema wakiwa wanashangiliwa na mashabiki.

“Wachezaji wetu siku hizi wamekua wakicheza vizuri kukiwa na mashabiki wakuwashangilia, ni kama wanacheza na akili zetu vile. Fuatilieni hilo mtalioa,” Haji Manara

“Kesho twendeni uwanjani tukashangilie timu yetu, hata kama itatokea bahati mbaya tumefungwa itakua ni sehemu ya mchezo maana wakati mwingine mpira una matokeo ya kikatili. Hata tukikosa matokea tusinyoosheane vidole kwamba amefungwa Ndimbo (Afisa habari wa TFF), Wilfed Kidao, rais Wallace Karia na wachezaji.” Alisema

Kikosi cha Stars kikiwa mazoezini kujiandaa na michezo ya kufuzu Afcon.

Katika mchezo wa kesho utakaopigwa saa moja usiku tayari Shirikisho la Soka lilishatangaza viingilio ambavyo ni 3000 mzunguko na 5000 VIP A&B.

Stars mpaka sasa ina alama moja baada ya kutoka sare dhidi ya Niger ugenini ikishika nafasi ya pili nyuma ya kinara Algeria mwenye alama tatu baada ya kuifunga Uganda.

Sambaza....